SABABU RASMI ZA MGAWANYIKO WA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE – (Sehemu ya I)
SURA MPYA YA BLOG NA MAMBO MAPYA!!!
Mengi yamesemwa sana kuhusiana na kuparanganyika kwa
kundi hili na hatimaye kutokea Wenge zaidi ya sita huku mbili kubwa ya
JB Mpiana na ya Werason zikionyesha upinzani wa hali ya juu.
Kuanzia wiki hii nitakuwa nikiwalete Makala ya
Historia Ndefu ya WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA
MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE. Ilikujua nini Hasa kilitokea baada ya
kupata mwanya wa mmoja wetu kuongea na mtunzi wa kitabu cha Historia
hiyo. Makal hizi zitakuwa zikikujia Kuanzia leo Jumatatu, Jumatano na
Ijumaa ikiwa ni muendelezo, hivyo usikose kupita hapa Jumatatu, Jumatano
na Ijumaa, kujua kwa undani nini kilitokea na kusababisha bendi hii ya
kizazi cha nne cha Musiki wa Congo kuparanganyika, ungana nasi kwenye
masimulizi haya ya kusisimua EXCLUSIVE. Shukrani za kipekee kwa Hadji Le Jbnique kwa kukokotoa na kutohoa habari hii mpaka leo unaisoma wewe, Respect Grand Rapids nakati ya USA.

Kitabu kitakua katika lugha mbili,kitakua mkifaransa
na mkilingala lakini nimejaribu kumshawishi akiweke pia mkingereza ili
watu wa afrika mashariki pia waweze kukisoma na kukielewa kwani
nimemueleza kwamba pia sehemu hizo na zambia,malawi,zimbambwe ambako
wanaongea zaidi english wapo wanafamilia wengi sana wenge,ameniahidi
kulifanyia kazi hilo,hivyo likifanikiwa nadhani itakua ni fursa nzuri
hata kwa wasiojua french au lingala kufahamu kilichojiri hasa kwa kuwa
mwandishi amejitahidi sana kuzungumza na wahusika wakuu wa iliyokuwa
wenge musica original kuanzia wanamuziki viongozi mpaka wanamuziki wa
kawaida,mapromota mpaka maproducer na wadau wa karibu sana.
So stay tuned,kama kawaida yetu hapa,habari zote za muziki na wanamuziki wa congo na kinachoendelea katika muziki wa congo kila wakati sisi tutakua wa kwanza kuzipata zikiwemo hizi za kitabu hiki.
Lakini kwa kuwa nilifanya nae mazungumzo ya kina
muhisika wa kitabu hiki,leo nitadodosa kidogo yaliyomo ndani ya kitabu
hicho kwa kuwa nimefanikiwa kuzipata dondoo zake,ila naomba kudiclare
interest kabla ya kuanza kwamba mimi ni mnazi mkubwa wa JB japo
simchukii WERRA pia,ila kwa kuwa leo nimeruhusiwa kukaa kwenye jukwaa
hili la heshima hapa juu joho langu la ushabiki naliweka kando ili
niweze kuwa fair,hivyo mtaona sehemu ambazo jb atakua alichemsha
nitamgonga bila kujali,sehemu ambazo werra alikua right nitampa credit
zake bila hiyana.Twende pamoja sasa:

WENGE iligawanyika na kusambaratika vipande viwili
mwaka 1997 December kufuatia sintofahamu kati ya JB MPIANA na WERRASON,
Huo ndio ukweli japo unauma. Yapo mambo mengi yalizungumzwa na
yanaendelea kuzungumzwa kufuatia hiyo sintofahamu iliyopelekea mtafaruku
huo wa mafahali hao wawili,wengine wakidai chanzo alikua ni
mwanamke,wengine wakidai JB MPIANA alikua akikerwa na udhaifu wa
WERRASON Katika udhibiti wa mapato ya bendi (werrason alikua ndio mtunza
fedha wa bendi ikumbukwe) lakini pia kuna wengine wamekua wakidai
chanzi ilikua ni chokochoko za Mzee Papa Wemba na Koffi Olomide ambao
inasemekana walikua wakiionea wivu wenge kutokana na kuwa iliundwa na
vijana wadogo wakati lakini ikawa haikamatiki kwa mafanikio.
Yote yanaweza kuwa majibu lakini sababu hasa
iliyopelekea sintofahamu hiyo na hatimaye wenge kusambaratika kwa mujibu
wa wahusika wenyewe ilikua ni mambo mawili,kwanza kabisa mafahali hao
wawili iligundulika kwamba ni vigumu kwao kufikia malengo na matarajio
yao ya hali ya juu waliyokua wameshayaingiza vichwani mwao wakiwa
pamoja,kila mmoja alitaka kumpanda mwenzie kichwani awe mkubwa yeye,na
jambo la pili alikua ni producer wao SIMON SIPE,yeye aliona anapata
hasara ku deal na lundo la viongozi
6!(JB,WERRA,MAKABA,MASELA,DOMINGUEZ,BLAIZE BULA) ambao ukifanya nao kazi
wote walikua wakihitaji treatment sawa, sasa ili kubana matumizi akaona
ni bora kwa upande wake awepo kiongozi mmoja ambae atakua anadeal nae
kwa ajili ya kushughulikia mambo mbalimbali yahusuyo production,na
mapato yatokanayo na concerts na mauzo ya cd ambayo pia yalikua
yakisimamiwa na SIPE,Hapa ikjitokeza kitu inaitwa Less Leaders Mo
Money…!
Kwa hiyo mwanzoni mwa 1998,WENGE BCBG ikazaliwa
ikijulikana mwanzoni kama WENGE MUSICA BCBG Lakini baadae wakaondoa neno
MUSICA kutokana na kwamba Didier Masela ambae ndio muanzilishi wa hilo
jina hakuwamo kundini humo,yeye alibaki na Adolphe na Werra,wakaamua
kumuachia MUSICA yake.Sasa mpaka hapa tunaona BCBG ndio ilikua bendi ya kwanza ku exist,
Hivyo ili kutochanganya mambo nitaizungumzia kwanza miaka mitatu ya mwanzo ya BCBG then MAISON MERRE nitamaliza nayo.
Usikose Jumatano kwa kujua kwa undani kuhusu miaka mitatu ya Wenge BCBG ya JB Mpiana na kuondoka kwa watu kama Dominguez, Aimelia, Ali Mbonda na wengineo. Kama una lolote tuandikie piusmicky@yahoo.co.uk au tuma sms 0713 666616.
Hapa nitakuacha na kibao cha Promesse bouboule ikiwa
ni utunzi wake shujaa Allain Mpela, hiki ni moja ya vibao
vilivyowatambulisha kwenye jukwaa la muziki kitaifa na kimataifa. Salamu
zangu za dhati kwako Big Producer Maghambo, Hadji Le Bcbgeeque,
Jema Mandali nakati ya USA, Papaa Julie We Eston Ndenge nini Papaa,
Mamaa Salma Jaruf nakati ya London, na funs wote wa Blog yangu nawatakia
Eid El Fitr Njema. .
Pius Uko juu sana
Asante sana bwana muandishi
Fred Mosha
Man of Style
Kumbuka, Papa Wemba ni mshauri ama alikuwa ni mshauri mkubwa wa Mpiana mpaka Mpiana alimshirikisha katika ile albamu yake ya Ndombolo na kuimba naye wimbo mmoja wa Calvaire Solitaire.
Kwa kila Mcongolais (Mzaire) anajuwa kuwa Mpiana ndiye aliyekuwa chanzo cha kuvunjika Wenge kwani alikuwa anaringa sana na alikuwa hana tungo nzuri zaidi ya ile ya Kin Ebouger (1990-1991). Alikuwa anaringa kwa sababu alikuwa na mashabiki lukuki kwa ajili ya uchezaji na uchekeshaji wake.
Tungo kali za BCBG zilitungwa na Blaise Bula Engineer ama La Voix Du Wenge (sauti ya Wenge), na Werra.
Ni kweli Wenge walikuwa na viongozi 6 na kila mmoja alitaka utawala. Wenge ilikuwa doomed kuvunjika kwani wakati ulifika watengane na ndiyo maana walikuwa wanafanyiana vituko kwani baada ya Makaba kutoa albamu yake minong’ono ikaanza ndani ya kundi. Wengi walimlaumu sana Makaba kwa kutoa ile albamu ila Mpiana aliunga mkono kwani naye pia alifuatia kufanya hivyo kwa kutoa ile albam yake ya Ndombolo Ya Solo.
Na baada ya hapa ndipo uhasama ukaanza kwani kina Makaba (swahiba wa Mpiana), na Blaise Bula wakawa upande wa JB Mpiana, kina Chouchou de Tout Le Monde (Ado Dominguez Ebondja Elongo) na President Masela wakawa upande wa Werra.
Ikumbukwe kuwa Mpiana siyo muasisi wa Wenge Musica. wasisi wa Wenge ni Masela President na Werra, Mpiana alikuja Wenge baada ya muda kidogo na alikuta bendi imejijenga tayari.
Baada ya mtafaruku wa muda mrefu ndipo Werra na masela wakahamua kuachana na Mpiana na kundi lake na wao kuunda Wenge Musica Maison Mere (yaani Wenge Musica ya asili ama Mama ya Wenge) kwani waasisi ni hao kina Masela na werra siyo Mpiana.
Baada ya kusambaratika kwao, kina Blaise Bula na Makaba nao wakatoka kwenda kuunda Wenge zao na huku kina Masela na Dominguez wakatoka kwenda kufanya hivyo hivyo.
Ila kwa bahati mbaya katika Wenge zote hizi ni Werrason pekee ndiye aliyeweza kudumu mpaka leo hii nakuandikia huu ujumbe. Mpiana toka 2005 hana jipya ni kama kaishiwa na hapa Kin watu wameshaanza kumuona mbabaishaji tu. Yeye hupiga nyimbo za matangazo ya bia tu na promosheni lakini hamna kipya kwake.
Binafsi namfagilia sana Engineer Bula ila naye kwa bahati mbaya naona kaishiwa siku hizi si kama yule wa enzi zile za Ave Maria.
Ninayo stori ndefu sana ya Wenge ila siwezi kubandika hapa mpaka nione hiko kitabu na kukisoma. Ahsanteni!
Kumbuka hapa tumeongelea Miaka mitatu ya hizi Wenge Mbili na Sababu ya Werason na JB Mpiana kutengana.
Karibu Sana
Papa wemba kweli alikua mshauri wa JB lakini na Koffi le Rambow du Zaire nae alikua msahuri wa Werra pia japo siku hizi wamekua ndio maadui wakubwa.
Alieivunja wenge SIMON SIPE,Werra na Jb walitumika tu.Jb hakua muanzilishi sawa tunakubali wote wala hakuna asiejua hilo,yeye alikuja baadae,lakini je kabla ya kuja Jb wenge ilikua inajulikana na nani?ilikuwaje bendi ikawa kimya mpaka Jb alipokuja kuitoa mafichoni na MULOLO na KIN E BOUGE yake?na je ilikuwaje kina Werra waanzilishi mpaka wakampisha wakuja JB awe kiongozi wao?unadhani kwa nini walikubali kutawaliwa na mgeni?
Halafu unasema Werra na Masela walitoka kwenda kuanzisha Maisono Merre,halafu badae eti Adolphe akatoka kwenda kuanzisha wenge tonya tonya,hapa unachanya mambo,Adolphe alitoka pamoja na kina Werra na Didier Masela Kwenda kuianzisha hiyo Maison Merre,japo Werra baadae aliwazunguka wenzake kwa kuwatumia vijana kuwahujumu kina Adolphe,mpaka kuna wakati ilikua paris kwenye concert vijana wa werrason kina Bill clinton walimvizia Adolphe na kubandika Big G kwenye Kiti chake huko back stage ili akikalia big g nguo iharibike ashindwe kupanda stejini werra atawale pekee yake,kaa hapa zipo stori nyingi zinakuja huko mbele u will see things,utaona mpaka Marquis de maison merre ilivyozaliwa.Tatizo Werra kwenye mambo ya hela anapunja sana.
Jb hana kitu zaidi ya matangazo ya bia,hii nayo kali,ina maana huko kinshasa album mpya ya jb soyons serieux haijafika bado?
Aaah poa bwana ni mtazamo na mahaba yako lakini
Yes Mpiana alikuja Wenge baadaye na kutoa changamoto kwenye nyimbo zake za awali. Wenge ilianzishwa mwaka 1983 na ikawa mafichoni miaka yote hiyo. Katika kipindi hiki walitoa nyimbo nyingi tu underground kwani bado walikuwa wachanga mno na walikuwa hawajapata a big break yet.
Kama sijakosea, kuna siku moja nafikiri mwaka 1987 mishoni ilitokea tamasha moja la muziki wa Jeune Vedette hapa Kinshasa na Wenge chini ya kina Aime Buanga, Ya JB Papa na Daida, Werra, Bula, Ado Dominguez na wengineo walitoa fora sana pale Commune Societe de Bandal (Bandalungwa). Na mwaka uliofuatia wakaalikwa kwenye Television national OZRT na kuanza kutambulika kwa fujo kwani kipindi hiki bendi nyingi zilikuwa zikiishi Ulaya na ngome ya Zaiko Langa Langa ilisambaratika na muziki ule wa lika la Zaiko (Papa Wemba, Bozi Boziana, Evoloko Jocker, Le Grand Zaiko Wawa, Minzoto, Choc Stars ya Ben Nyamabo, Victoria Eleison) nyinginezo nyingi tu zilikuwa zinafifia.
Hapa ndipo Wenge ikapata a big break. Kwani walikuja na nyimbo kama vile Mulolo (JB Mpiana), Ave Maria (Ya Blaise Bula), A Moi Nicky D (Werrason)…yaani palikuwa patamu sana, na walikuja na ule mtindo wao wa Bouger, Bouger…..ah Kin na biso…mawa trop, yaani kweli ilikuwa raha tupu kipindi kile.
Nirudi kwenye makala yako ama majibu yako.
Nilisema kina Werrason, Masela, na Tata Mobitchi (Dominguez) walijiengua na kuanzisha Wenge Musica Maison Mere na kumuachia JB na Wenge BCBG.
Pale Maison Mere nako Werra alikuwa anabania sana pesa na kukosana na Dominguez kitendo kilichomfanya naye ajitoe kwenda kuunda bendi yake mwaka 2001.
Mkaba yeye hutoa albam zake kama a solo artist ila anajiita kama Makaba Du Wenge Musica ili atambulike zaidi kibiashara. Na Blaise Bula naye anafanya hivyo hivyo. Bula bendi yake inaitwa Ponderation 8 ya Ingineur Blaise Bula de Wenge Musica.
Kiukweli ni kwamba kuna Wenge Musica ama Wenge 5 tu ndizo zinazofahamika.
(1) Wenge Musica ya Mpiana (Wenge Musica BCBG)
(2) wenge Musica ya Werrason (Wenge Musica Maison Mere)
(3) Wenge Musica ya Marie Paul (Wenge Musica Aile Paris)
(4) Wenge Musica ya Aime Buanga (Wenge Musica Kumbela)
(5) Wenge Musica ya Tata Mobitchi (Wenge Tonya Tonya)
Nimechoka kuandika naishia hapa. Ila tambua kuwa hii bendi ya Wenge ilikuwa doomed kufa kwani werra na Mpiana walikuwa na vita bariidi miongoni mwao haswa kwa kuwa Mpiana si muasisi wa wenge na yeye Mpiana ndiyo alitaka atambulike kama muasisi wa Wenge kitu ambacho kilimkera werrason.
Hivi huyu jb alikua na nguvu kiasi gani na ujasiri wa namna gani kiasi awakute watu tayari na kitu chao then yeye aliyeletwa tu tena kaletwa na makaba ambae nae alikua wakuja pia aweze kuwaovertake waasisi wote na yeye kukaa mbele na bendi kuendelea kutoa album na kupiga shows since 80’s mpaka 90’s bila ridhaa ya hao waasisi?hii katika hali ya kawaida haiwezekani japo tuko mbali na kinshasa.
Mimi nasema hivi…kama unamuona mbwa yuko juu ya mti usiulize amepandaje uliza nani alimpandisha kwani katika hali ya kawaida mbwa hawezi kupanda juu ya mti bila kupandishwa.
Melesi mingi.
“Baada ya mtafaruku wa muda mrefu ndipo werra na masela wakaamua kuachana na mpiana na kundi lake na wao kuunda wenge musica maison mere” mwisho wa kunukuu.Sasa nataka kujua haya maneno uliyaandika wewe mwenyewe au kuna mtu aliyagushi na kupoteza maana uliyokusudia?Maana hapo hatujaona jina Adolphe Dominguez likitajwa kwenda kuanzisha maison mere.
Then ukaendelea kuandika nanukuu tena:
“Baada ya kusambaratika kwao,kina Blaize Bula na Makaba nao wakatoka kwenda kuunda wenge zao na huku kina Masela na Dominguez wakitoka kwenda kufanya hivyo hivyo”.mwisho wa kunukuu.Sasa soma sawa maandishi yako halafu upime mwenyewe kama hukustahili kujibiwa vile.
Jb mpiana anapitwa mpaka na Kabose Bulembi na hiyo “ELECTION” yake aliyoirelease! hapa sina comment
Ila kuna mahali naomba nichangie kidogo,umesema wenge walimlaumu makaba ku release solo album,hapa nadhani unamaanisha ile album ya “POILE OU FACE” mwaka 1995 .Walimlaumu kwanini sasa?hukutufafanulia.Mi nadhani labda ungesema Werrason alimlaumu makaba kwa hiyo album labda japo mimi sijawahi kusikia hilo.Lakini iweje wamlaum,mbona yeye alifanya hiyo album kwa kuwashirikisha watu watatu tu toka wenge,ambao ni Titina,Le grand chibuta roberto ekokota na jb,wengine hawakuwa member wa wenge maana alimshirikisha mzee Sam mangwana,Dindo yogo,Luciana Demingongo,Abby Suriya,Ballou Cante na King Kester Emeneya ambae wengine wanamwita victoria eleison sijui kwanini.
Halafu JB hajawahi kutoa album inayoitwa ndombolo labda unamaanisha Feux de L’amour,tukubali tukatae mitafaruku ndani ya wenge haikua baina ya werra na jb tu,kama mfuatiliaji wa mambo hapo kin december 1997 sijui kama ulikua umeshaingia congo,ndani ya Grand Kin Hotel kulifanyika concert ya wenge ambayo hakuna mpenzi wa muziki hasa wa wenge ndani ya congo ataisahau maana concert hiyo in all names ikabatizwa
as “concert de la separation” baade, Tafuta video uone kilichotokea baina ya werra na blaize bulla mbele ya papa wemba ambae alikuja hapo kama mualikwa,Kiufupi tu ni kwamba Sele na Werra siku hiyo walitukanana sana,Sele akamwambia Werra maneno hayo “rafiki yangu kila siku unaota uwe kama mimi,uwe kama Jb,uwe kama Makaba,hizo ni ndoto kaka yangu” mwisho wa kunukuu.Hapo ndio utaona vile joto lilivyokuwa kali kundini humo kwa wanamuziki wote sio issue ya werra na jb pekee kama unavyodai.Otherwise tuko pamoja cuz constructive criticism are most welcome to me alwayz
WENGE NI BAND ILIOKUWA NA MUSICIE WENGI …ILA IKUMBUKWE KWAMBA KATIKA HAWA MUSICIE JB ALIKUWA MASIKINI NA DECATION YAKE KWA BAND NA USISAHAU VOCAL(SAUTI) NDIO ILIMUWEKA MBELE…MFANO MUDOGO.MUNAJUA KOFFI NA PAPA WEMBA WALIKUWA KWENYE BAND MOJA,LAKINI PAPA WEMBA ALIKUWA JUU SANA SHAURI YA SAUTI YAKE NA KOFFI ALIFUNIKWA NA SAUTI YA PAPA WEMBA..KOFFI ALIONDOKA NA AKAJARIBU KUPIGA MUSIKI AMBAO ULIKUWA MUSIKI WA POLE POLE SANA…
NIRUDI KWA JB NA WERA…JB SAUTI YAKE NDIO ILIMUWEKA
PALE NA NIUKWELI MABOSS WALIKUWA WENGI NA YEYE JB HAKUKUWA NA FARANGA HIVO ALIANZA KUPATA PESA ZAIDI NAKUFUNIKA WENGINE..
ILE KUSEMA JB HAKUWA NA NYIMBO MUSURI SI KWELI…PALE ALIPOTOA MIMBO YA Feux de Amour http://www.youtube.com/watch?v=tX6T1QCNA8M&feature=related
PIA WATU WENGI CONGO WALIKUWA WANASEMA JB TALENT YA KUANDIKA MIMBO SASA ALISEMA ATAFANYA NYIMBO NYINGI SANA..NA WENGI WALISEMA WENGE YA JB INGEKUFA LAKINI ALIJITAIDI NAKUPATA CONTRACT KATIKA COMPANY ZA BEER KABLA YA MUSICIAN YEYOTE CONGO…
PRACTICE KATIKA BAND YEYOTE NI MUHIMU SASA WERRA HAKUKUWA AKIWAPO NA HIYO ILIFANYA BAND YAO YA MWANZO HAIKUKUWA NA ALBAM NYINGI NA JB ALIPENDA KUTOSHA ALBAM NYINGI…
SIKU INGINE WAPENDWA…SOTE TUNAPENDA MUSIC WA WERRA NA JB ..FERRE GOLLA NA WENGINE
MUKONGO
ONA JB http://www.youtube.com/watch?v=0uICVljMKKU&feature=related
HII NI ILE MIE NAPENDA KABISA UTAONA VILE SAUTI YA JB ILIKUWA NGUVUhttp://www.youtube.com/watch?v=lagiki_xlJ8&feature=related
Nanukuu “Kwa hiyo mwanzoni mwa 1998,WENGE BCBG ikazaliwa ikijulikana mwanzoni kama WENGE MUSICA BCBG Lakini baadae wakaondoa neno MUSICA kutokana na kwamba Didier Masela ambae ndio muanzilishi wa hilo jina hakuwamo kundini humo,yeye alibaki na Adolphe na Werra,wakaamua kumuachia MUSICA yake.Sasa mpaka hapa tunaona BCBG ndio ilikua bendi ya kwanza ku exist”,
Hapa sikubaliani na mwandishi, vile baada ya sintofahamu hiyo hawa watu waligawana vyombo na kila kitu kilichohusu bendi hiyo, na akina werra wakawa na haki ya kulitumia jina la Wenge Musica, mpiana na wenzie wakaamua kujiita wenge BCBG. Mpiana ndie alikuwa wa kwanza kutoa albam ikafuatiwa na werra mwezi mmoja baadae. hivo si kwamba BCBG ndio ilianza ku-exist.
Ametunga ama kuimba peke yale rhumba nyingi tu kama feux de l’amour, omba n.k
Jb akiwa na wenge original alifanikiwa kupata tuzo nyingi tu na si kwa Wera ambae hakupata tuzo yoyote.
hivi nambieni wera katunga ama kuimba wimbo gani peke yake? Bila msaada wa vijana?
Hivyo Jb mpiana ni mwamamuzi kamili. Hana kinyongo na ndio maana huwa anawakumbuka kwenye nyimbo zake hasa wa omba huwataja majina kina Afande, aimelia,tutu na makaba vipi wera anaweza kumtaja ferre?
Mnakumbuka nyimbo kama masua, education, bana lunda, calvairem solitare, top module nk
Jamaa yuko juu sana acha aitwe mukulu.
Yuko juu ya wera hivi wakipigiwa vyombo waimbe na wera bila kushirikisha waimbaji wengine wera ataimba wimbo upi peke yake?
I really found you by mistake, while I was searching
on Aol for something else, Regardless I am here now
and would just like to say thanks for a incredible post and
a all round interesting blog (I also love the theme/design), I don’t have
time to read through it all at the moment but I have book-marked it and also added your RSS feeds,
so when I have time I will be back to read much more, Please do keep
up the great b.
Kama tulivyoona sababu kubwa ya kusambaratika kwa wenge ni pesa, basi pesa hizo hizo zinaweza kuwakusanya wenge musica bcbg 4×4 wakafanya shoo moja tu katika sehemu ambayo promota ataona inafaa sjui ni wapi kuna mashabiki wengi wa wenge? labda Dar es salaam??
Hitimisho: Hata wao Mpiana na Werra wanaogopana na ndio maana kwa sasa ni marafiki sana kuliko hata wale waliokuwa nao kwenye bendi zao.
Ahsante
Hitimisho: Hata wao Mpiana na Werra wanaogopana na ndio maana kwa sasa ni marafiki sana kuliko hata wale waliokuwa nao kwenye bendi zao.
Ahsante
Ushauri wangu ni huo kwanini sisi wana wenge family tusianzishe kitu chetu Fulani ili na wapenzi wengine watuige? naomba maoni yenu mnasemaje wadau?
Contact: Mimi nipo Tanzania Dar es Salaam
sehemu ya MBEZI LUIZ
Karibuni sana.