Huha Makuja Nyungi (kushoto), akiwa anaelekea mahakamani muda mfupi kabla ya kusomewa hukumu hiyo. Kulia ni mtuhumiwa mwingine katika kesi hiyo
Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Simiyu, imemhukumu kutumikia kifungo cha miaka 40 jela mkazi mmoja wa huyo ni mkazi wa kijiji cha Girya, mkoani humo, huku Jeshi la Polisi likiwashikilia watuhumiwa wengine wawili, kutokana na kukutwa na nyara za serikali pasipokuwa na kibali cha Mkurugenzi wa wanyama pori.
Huha Makuja Nyungi, mwenye umri wa miaka 28, alihukumiwa kifungo hicho baada ya kukiri makosa ya kuhusika na kosa la kukutwa na nyara hizo, mbele ya Hakimu Mfawidhi John Nkwabhi.
Bw. Nyungi, pamoja na wenzake wawili ambao majina yao hayakuweza kupatikana haraka, walikamatwa kufuatia msako mkali ulioendeshwa kwa ushirikiano baina ya askari wanyamapori na taasisi ya Serengeti Wildlife and Conservation, ya mkoani Simiyu.
Katika msako huo, mali mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 50 za kitanzania, vikiwemo vipande zaidi ya 500 vya nyama ya nyumbu, ziliweza kukamatwa.
Akisoma hukumu hiyo, hakimu Nkwabhi, alisema anamhukumu mtuhumiwa adhabu hiyo ili iwe fundisho na onyo kwa watu wengine ambao wamekuwa wakijihusisha na uwindaji haramu, usiozingatia taratibu za kisheria.
Huha Makuja Nyungi (kulia akiwa na mtuhumiwa mwingine wa kesi hiyo, ambaye alirudishwa rumande kwa kuwa alikataa kushiriki kutenda kosa hilo
No comments:
Post a Comment