NA Berensi Alikadi-Musoma
MKAZI mmoja wa kijiji cha Maneke kilichoko kata ya Tegeruka wilaya ya Musoma,Magwegwe Chiriso 36 amelazwa katika hospital ya mkoa wa Mara baada ya kuvamiwa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi na kisha kumpora kiasi cha shilingi laki tisa.
Akiongea na mwandishi wa habari hizi jana katika wodi namba 8 lililopo katika hosptali hiyo Magwegwe amesema kuwa tukio hilo limetokea Agost 20 mwaka huu majira ya saa 6 usiku ghafula alisikia mlango ukikongwa na jiwe kubwa maarufu kama Fatuma.
Alisema kuwa baada ya majambazi hao kubomoa mlango huo waliingia ndani majambazi wawili wakiwa na silaha za jadi ambapo walimuamilisha yeye na mke wake wake wawape pesa kiasi cha shilingi laki saba huku wakiwakata kata kwa mapanga.
Magwegwe alifafanua kuwa baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya aliwaambia kuwa pesa ziko sandukuni ambapo walibomoa sanduku na kuchukuwa kiasi cha shilingi laki tisa na kisha wakaotokomea kusikojulikana.
Alifafanua kuwa baada ya kuona wameondoka yeye na mke wake walipiga yowe ambapo majirani walifika na kuwachukuwa hadi katika kituo cha polisi Musoma ambako walipewa fomu namba 3 na kisha kwenda kutibiwa katika hospital hiyo ambako amelazwa yeye na mke wake. Wakiendelea na matibabu.
Mhudumu wa zamu katika wodi hilo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwa madai kuwa yeye si msemaji wa hospital hiyo amesema kuwa hali za watu hao zinaendelea vizuri.
Akizungumzia tukio hilo kwa niaba ya kamanda wa polisi wa mkoa wa Mara,mkuu wa upelelezi wa mkoa huo Emanuel Lukula amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa polisi bado wanaendelea kufanya upelelezi ili kuwabaini wale wote waliohusika na tukio hilo ili waweze kufikishwa mahakamani.
MWISHO
No comments:
Post a Comment