Wednesday, August 29, 2012

MWALIMU WA KIISLAMU KOTINI KWA KUGOMA KUHESABIWA

Kortini kwa kugoma kuhesabiwa

na Jovither Kaijage, Ukerewe

MWALIMU wa dini ya Kiislamu, Mohamed Iddi (25), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ukerewe, Mwanza akikabiliwa na shitaka la kupinga kuhesabiwa.
Iddi, mkazi wa Kiloleli, alifikishwa mahakamani hapo na kusomewa shitaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Rouben Luhasha.
Akimsomea shitaka hilo, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Inspekta Samwel Onyongo, alidai Agosti 26 mwaka huu, katika nyumba ya kulala wageni ya Baba Kapaya iliyoko kitongoji cha Mviringo A, mjini Nansio, mshitakiwa kwa makusudi alikataa kutoa taarifa zake kwa karani wa sensa ya watu na makazi, John Msafiri aliyepewa wajibu huo kwa mujibu wa sheria.
Mshitakiwa alikana tuhuma hizo na amepelekwa rumande baada ya kukosa wadhamini. Kesi itatajwa Septemba 11, mwaka huu.
Kwa mujibu wa sheria, mtu akithibitika kutenda kosa hilo na mengine ya namna hiyo atahukumiwa kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini ya sh 600,000 au adhabu zote mbili kwa pamoja.
Katika tukio jingine, baadhi ya makarani wa sensa wilayani Ukerewe, wameishiwa vifaa hasa fomu za kujaza taarifa za watu, hali inayoweza kuwa kikwazo kingine katika kufanikisha sensa hiyo.
Mratibu wa sensa wa wilaya hiyo, alisema hayo jana alipokuwa akitoa taarifa ya hali ya maendeleo ya sensa.
Alivitaja vifaa ambavyo vimeisha kuwa ni nakala 7,500 za dodoso refu na dodoso fupi nakala 10,000 ambapo baadhi ya vifaa zikiwemo kalamu 950 za wino wa bluu hazijapelekwa kabisa.
Alivitaja vifaa vingine vilivyopungua kuwa ni sare 875 za makarani wa sensa, vibao 50 vya kusiliba fomu pamoja na kalamu 50 zenye wino mwekundu.


kwa habari zaidi soma Tanzania daima  Agost 31

No comments:

Post a Comment

Comments System

disqus

Disqus Shortname

msora

Popular Posts

Header Ads

ad