Wachimba migodi ishirini na nane hawajulikani waliko kusini magharibi mwa Uchina baada ya mlipuko kutokea na kuwaua wafanyikazi wenzao kumi na tisa.
Shirika la habari la kitaifa nchini humo limesema kuwa makundi ya waokoaji kutoka migodi mingine waliweza kuwaokoa zaidi ya watu mia moja baada ya mlipuko wa gesi katika machimbo ya Sichuan .Takwimu rasmi za serikali zinasema kuwa takriban watu elfu mbili wameuawa katika ajali za migodi nchini Uchina ambazo zimetajwa kuwa hatari zaidi duniani.
Vifo hivyo pia vinasemekana kupungua katika miaka ya hivi karibuni japo waandishi wanasema kuwa huenda baadhi ya ajali zinakosa kuripotiwa.
No comments:
Post a Comment