Name:  Daudi na Kamhanda.jpg

Views: 0

Size:  78.4 KB

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka Iringa, inaelezwa kuwa muda mchache kabla ya marehemu Daudi Mwangosi hajafikwa na mauti (kulipuliwa na bomu) kulikuwa na hali ya kutokuelewana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda katika mahojiano baina yao wawili.

Inaelezwa kuwa Marehemu Daudi alikuwa akitaka kujua ni kwanini Polisi wanawazuia CHADEMA kukutana katika ofisi yao na pia kujua hatma ya katazo la mikutano ya kisiasa kwa jinsi zoezi la sensa lilivyo. Kamanda Kamuhanda akamjibu kwa swala kuwa anamuuliza hivyo yeye (Daudi) kama nani!?

Mahojiano yao hayakuwa na maelewano mazuri na inaelezwa kuwa Kamanda huyo anahusika na amri ya kumsulubu Mwandishi Daudi Mwangosi.

Picha hii inaonesha marehemu na Kamanda Kamuhanda wakiwasiliana kwa njia ya mahojiano. Hii ni muda mchache sana kabla ya Daudi kukamatwa na kusulubiwa na hatimae kulipuliwa na kinachoaminika kuwa ni bomu kiasi cha kusambaratisha mwili wa mwandishi huyo vipandevipande.
Click image for larger version. 



Name: Kamanda Kamuhanda.JPG 

Views: 0 

Size: 41.0 KB 

ID: 63687



Huyu ndie Kamanda Kamuhanda...
HUYU NDIYE MUUAJI MKUU KAMUHANDA. AMEDHIRISHA KUWA KAZI YAKE KUBWA SIYO KULINDA RAIA BALI KUUA KILA ALIYE KINYUME NA MATAKWA YA VIONGOZI JAMBAZI. Mtu wa namna hii unaweza kuelewa atakuwa ameua watu wengi kiasi gani mpaka kufikia cheo hicho. Mwuuaji hata ukampa cheo kikubwa kiasi gani, hamu ya kuondoa uhai wa binadamu wenzake haiondoki. Siyo vema kumwombea au kumtakia kifo binadamu mwenzio lakini ni ukweli ulio wazi kuwa japo hatutathubutu kuinua mikono yetu kumwua Kamuhanda, lakini kwa mauaji anayoyasimamia kwa makusudi, ni heri kwetu Muumba wetu angewatanguliza hawa kwanza ili Tanzania pawe mahali salama pa kuishi watu wote, wanyinge na wenye nguvu. Mwuumba wetu, hatutaki kuingilia kazi yako, lakini ukiona inafaa uwaondoe wauaji wa makusudi katika nchi yetu ili na wanyonge wapate kuishi kadiri ya ulivyowapangia.