
Makamu wa rais wa Iraq, Tariq al-Hashemi
Mahakama nchini Iraq imepitisha hukumu ya kifo kwa makamu wa rais, Tariq al-Hashemi, baada ya kumkuta na hatia kwa kuongoza makundi ya kuuwa watu, yaliyowalenga Washia na askari wa usalama.
Makamo wa rais, wa madhehebu ya Sunni, hakuweko mahakamani wakati wa hukumu hiyo kwani alishaikimbia Iraq awali mwaka huu, akiwa sasa anaishi Uturuki.
Kesi hiyo imezusha msukosuko wa kisiasa katika serikali ya Iraq, iliyogawa madaraka kati ya Wa-Sunni, wa-Shia na WaKurd.
Bwana al-Hashemi amemshutumu Waziri Mkuu Nuri al-Maliki ambaye ni M-Shia, kuwa anawasaka wapinzani wake wa kisiasa wa madhehebu ya Sunni, lakini serikali inasisitiza kuwa kesi hiyo inafuata misingi ya sheria tu
Chanzo BBC
No comments:
Post a Comment