
Mashambulizi dhidi ya ubalozi wa Marekani mjini Benghazi
Maafisa wa Marekani wanasema serikali ya nchi hiyo inachunguza ikiwa mashambulio ya jumanne kwenye ubalozi wa Marekani katika mji wa Libya wa Benghazi yalikuwa ni ya kupangwa au la .
Balozi wa Marekani nchini Libya , Christopher Stevens, aliuawa .Maafisa wa Marekani wameelezea mashambulio hayo kama yenye utata na yenye kupangwa kitaalamu na kuna tetesi kwamba makundi ya jihad huenda yalihusika .
Awali ilifikiriwa kuwa mashambulio hayo yalikuwa na uhusiano na maandamano ya kupinga filamu iliyokuwa inamkejeli Mtume Mohammed.
Takriban waandamanaji mia mbili wamekusanyika karibu na ubalozi wa Marekani mjini Cairo Misri kwa usiku wa pili kuelezea hasira yao juu ya filamu hiyo .

Aliyekuwa balozi wa Marekani nchini Libya Christopher Stevens
Watu wenye silaha waliokuwa na maguruneti walichomo moto jengo la ubalozi na walioshuhudia wanasema watu hao walizingira eneo hilo.
Rais Obama amelaani vikali shambulio hilo na ameahidi kushirikiana na serikali ya Libya kuwafikisha mbele ya sheria wahusika.
Chanzo BBC
No comments:
Post a Comment