Huyu askari alimwelekezea mtutu tumboni na kumsambaratisha marehemu. Ni wazi watu wa Iringa wanamfahamu askari huyu.
Pembeni ni shangingi la RPC, askari huyu naye kashuhudia kitendo hiki cha kikatili. Wanahabari tushirikiane kupiga kelele. Hapa walikuwa wamemaliza unyama wao wakimwondoa mwenzao aliyeumia eneo la tukio
Kama ni kesi, askari huyu anaweza kuhojiwa. Nimekata picha kusitiri mwili wa marehemu.
Marehemu kafa akipigania haki za wanahabari, ni wakati wa wanahabari kushirikiana vinginevyo wanasiasa wataendelea kutumia vibaya vyombo vya dola dhidi yetu.
No comments:
Post a Comment