Friday, September 14, 2012

RADI YAUWA MMOJA,YAJERUHI WAWILI-BUND


NA Berensi Alikadi-Bunda

MTU mmoja amefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa vibaya baada ya kupigwa na radi.

Akielezea tukio hilo jana kwa waandishi wa habari mwenyekiti wa kamati ya maafa ya wilaya hiyo Joshua Mirumbe alisema kuwa tukio hilo limetokea sept 12 mwaka huu majira ya saa 10 jioni katika kijiji cha Mikomariro tarafa ya Chamliho.

Alimtaja aliyekufa kuwa ni Marwa Magena 65 mkazi wa kijiji cha Masinki wilayani Serengeti ambaye alikuwa amefika kijijini hapo kwa ajili ya kusalimia ndugu yake ambaye anaishi katika hicho.

Mirumbe ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo alisema kuwa siku hiyo mvua kubwa ilikuwa katika kijiji hicho ambayo iliambatana na radi iliyompiga mtu huyo ambaye alikufa hapohapo.

Alifafanua kuwa pamoja na radi hiyo kuuwa mtu huyo pia iliwajeruhi watu wengine wawili,ambao ni Rbobhi Nyamhanga na Tiri Nyamhanga wote wakazi wa kijiji cha Mekomariro.

‘’Hawa wawili wamejeruhiwa vibaya na mmoja kati yao,Rhobi Nyamhanga amepelekwa Bugando kwa matibabu zaidi na mwenzake amelazwa katika hospital ya Butiama kwa matibabu zaidi,bado sijapata maendeleo yao nikipata nitawaambia’’alisema Mirumbe.

Hata hivyo mkuu huyo aliwatahadhalisha wananchi kuwa makini na mvua zinazoanza kunyesha ikiwa ni pamoja na kuweka nyumba zao imara ili zisije zikaezuliwa na upepo.
MWISHO

No comments:

Post a Comment

Comments System

disqus

Disqus Shortname

msora

Popular Posts

Header Ads

ad