Serikali ya Kenya imemfikisha mahakamani mtuhumiwa aliyehusika na ghasia za Mombasa kwa mashtaka matatu ya kuawaua polisi mjini humo. Hata hivyo upande wa mashtaka uliitaka mahakama kuwapa polisi siku kumi kukamilisha uchunguzi wao kuhusu ghasia hizo za Mombasa ambazo zilisababishwa na tukio la kuuawa kwa muhubiri wa kiislamu Aboud Rogo. Mtuhumiwa huyo kwa jina Majivuno Mwasambu alishtakiwa kwa kuhusika na kuwaua askari Kipchoge Kipkoech, Kithome Mgunyi na Abdul-Aziz katika eneo la Mwandoni mjini Mombasa. Askari hao watatu walikuwa ni wa sehemu ya kikosi cha polisi 16 waliokuwa wamekwenda kuzuia kanisa kuchomwa na vijana wa kiislamu waliokuwa wakiandamana kupinga mauaji ya sheikh Rogo mjini humo. Inasemekana bomu la mkono lilirushwa katika lori ambalo polisi hao walikuwemo na kusababisha vifo vyao. Sheikh Rogo ambaye anadaiwa kuhusika na shughuli za kigaidi nchini Kenya na Somalia, aliuawa na watu wasiojulikana wiki hii na kusababisha wafuasi wake vijana kufanya maandamano makubwa mjini Mombasa yaliyopelekea kuchomwa kwa makanisa mjini humo.
Habari hii kwa idhini ya radio china kimataifa
Habari hii kwa idhini ya radio china kimataifa
No comments:
Post a Comment