Saturday, September 1, 2012

Watu 30 wafa maji Guinea



Wakuu wa Guinea wanasema kuwa watu kama 30 wamekufa kwenye ajali ya mashua katika bahari ya Atlantic.
Ghuba ya Guinea
Inaarifiwa kuwa mashua hiyo ilikwenda mrama kwa sababu ya dhoruba wakati ikisafiri kutoka mji mkuu, Conakry, kuelekea kisiwa cha Kassa, safari ya kilomita 10.
Shughuli za uokozi zimesimamishwa.
Ajali kama hizo zinatokea mara kwa mara nchini Guinea na kwengineko Afrika, ambako mashua hupakia abiria wengi na hazitazamwi sawa sawa.
Habari hii kwa idhini ya idhaa ya BBC


No comments:

Post a Comment

Comments System

disqus

Disqus Shortname

msora

Popular Posts

Header Ads

ad