Wednesday, August 21, 2013

DIWANI AKABIDHI MADAWATI


NA Berensi Alikadi-Tarime.
21/8/2013
DIWANI wa kata ya Turwa wilayani Tarime,Ndesi Mbusiro[CHADEMA} juzi alikabidhi madawati 8 na viti 13vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni moja katika shule ya msingi Tagota iliyoko katika kata ya Turwa wilayani hapo.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa uongozi wa kijiji hicho pamoja na kamati ya shule hiyo diwani huyo alisema kuwa hiyo ni mojawapo ya ahadi alizoahidi katika shule hiyo wakati alipokuwa akiomba kura kwa wananchi wa kijiji hicho.
‘’Ndugu zangu ahadi ni deni nilipotoa ahadi katika shule hii kila nilipokuwa nikipita dhamira ilikuwa ikinisuta lakini leo nafurahi kwaambia wazazi na waalimu kuwa kile nilichokoahidi nimekitimiza na siyo hicho tu bali hata vingine ambavyo niliahidi nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu ili niweze kutimiza’’alisema Ndesi
Alisema kuwa ana imani kuwa madawati hayo yatawasaidia wanafunzi wa shule hiyo ambao walikuwa na upungufu wa madawati ambapo pia viti hivyo vitawasaidia waalimu wa shule hiyo.
Awali mwalimu mkuu wa shule hiyo,Samweli Magoiga alisema kuwa shule hiyo illkuwa inakabiliwa na upungufu wa viti 32 na meza 43 na madawati139 hali ambayo imekuwa ikisababisha wanafunzi wa shule hiyo pamoja na waalimu kukaa kwa shida.
Alisema kuwa mapungufu mengine ni pamoja na uchakavu wa majengo na nyumba za waalimu na tatizo la umeme jambo alililomuomba diwani huyo alisimamie ambapo alisema kuwa wataendelea kuvifanyia marekebisho kadiri watakavyokuwa wanapata fedha toka halimashauri ya wilaya hiyo na kwa wafadhili.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamempongeza diwani huyo kwa kutekeleza ahadi yake na kwamba vifaa hivyo vitawasaidia waalimu na wanafunzi.
Mwenyekiti msitaafu wa kijiji hicho na mwenyekiti wa CCM kata ya Turwa,Eliakim Mwitentya alisema kuwa kiongozi bora ni Yule anayefanya kazi kwa vitendo hata kama anatoka chama cha upinzani na kwamba diwani huyo ameonyesha uongozi wa vitendo.
Naye mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Raheli Mwema amewataka waalimu wa shule hiyo kuvitunza ipasavyo kwani kuna baadhi ya shule zingine zimekuwa hazitunzi vifaa vya shule yakiwemo madawati na viti
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo waliongea na gazeti hili walimpongeza diwani huyo na kwamba watajitahidi kusoma kwa bidii kwani wamepata madawati mazuri ambayo yatasaidia kusoma wakiwa wamekaa pasipo na tatizo
Mwisho

No comments:

Post a Comment

Comments System

disqus

Disqus Shortname

msora

Popular Posts

Header Ads

ad