NA Berensi Alikadi-Tarime.
21/8/2013
DIWANI wa kata ya Turwa wilayani
Tarime,Ndesi Mbusiro[CHADEMA} juzi alikabidhi madawati 8 na viti 13vyote vikiwa
na thamani ya shilingi milioni moja katika shule ya msingi Tagota iliyoko katika
kata ya Turwa wilayani hapo.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa
uongozi wa kijiji hicho pamoja na kamati ya shule hiyo diwani huyo alisema kuwa
hiyo ni mojawapo ya ahadi alizoahidi katika shule hiyo wakati alipokuwa akiomba
kura kwa wananchi wa kijiji hicho.
‘’Ndugu zangu ahadi ni deni
nilipotoa ahadi katika shule hii kila nilipokuwa nikipita dhamira ilikuwa
ikinisuta lakini leo nafurahi kwaambia wazazi na waalimu kuwa kile
nilichokoahidi nimekitimiza na siyo hicho tu bali hata vingine ambavyo
niliahidi nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu ili niweze kutimiza’’alisema Ndesi
Alisema kuwa ana imani kuwa
madawati hayo yatawasaidia wanafunzi wa shule hiyo ambao walikuwa na upungufu
wa madawati ambapo pia viti hivyo vitawasaidia waalimu wa shule hiyo.
Awali mwalimu mkuu wa shule
hiyo,Samweli Magoiga alisema kuwa shule hiyo illkuwa inakabiliwa na upungufu wa
viti 32 na meza 43 na madawati139 hali ambayo imekuwa ikisababisha wanafunzi wa
shule hiyo pamoja na waalimu kukaa kwa shida.
Alisema kuwa mapungufu mengine ni
pamoja na uchakavu wa majengo na nyumba za waalimu na tatizo la umeme jambo
alililomuomba diwani huyo alisimamie ambapo alisema kuwa wataendelea kuvifanyia
marekebisho kadiri watakavyokuwa wanapata fedha toka halimashauri ya wilaya
hiyo na kwa wafadhili.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi
wa kijiji hicho wamempongeza diwani huyo kwa kutekeleza ahadi yake na kwamba
vifaa hivyo vitawasaidia waalimu na wanafunzi.
Mwenyekiti msitaafu wa kijiji
hicho na mwenyekiti wa CCM kata ya Turwa,Eliakim Mwitentya alisema kuwa
kiongozi bora ni Yule anayefanya kazi kwa vitendo hata kama anatoka chama cha
upinzani na kwamba diwani huyo ameonyesha uongozi wa vitendo.
Naye mwenyekiti wa kamati ya
shule hiyo Raheli Mwema amewataka waalimu wa shule hiyo kuvitunza ipasavyo
kwani kuna baadhi ya shule zingine zimekuwa hazitunzi vifaa vya shule yakiwemo
madawati na viti
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo
waliongea na gazeti hili walimpongeza diwani huyo na kwamba watajitahidi kusoma
kwa bidii kwani wamepata madawati mazuri ambayo yatasaidia kusoma wakiwa
wamekaa pasipo na tatizo
Mwisho
No comments:
Post a Comment