-Aliamua
kwenda kujisalimisha polisi baada ya kutoka gerezani.
Na Berensi
Alikadi.
1.9.2013
MAKUYU Magai
ni mkazi wa mtaa wa Nyakato katika manispaa ya Musoma,alizaliwa mwaka 1973 huko
katika kijiji cha Murangi wilaya ya Butiama mkoani Mara.
Baada ya
kuhitimu masomo yake ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Somanya iliyoko katika kijiji cha Mugango wilaya hiyo
ya Butiama mwaka 1993 aliamua kufanya shughuli mbalimbali za ujasiliamali baada
ya matokeo yake kutokuwa mazuri hivyo kushindwa kuendelea na masomo ya juu.
Mnamo mwaka
1996 aliamua kwenda mjini Musoma na kuweka makazi yake mtaa wa nyakato maziwa
ambapo aliamua kuanzisha ukumbi wa kuonyesha picha ambayo ndiyo shughuli ambayo
ilikuwa ikimpatia kipato.
Magai
anasema akiwa katika shughuli hiyo alishawishiwa na baadhi ya wezi ambao
walikuwa wakiiba vitu mbalimbali na kumuuzia
kazi ambayo aliianza mwaka 2000.
Anasema
baada ya kuendelea na shughuli hiyo hatimaye aliangukia kwenye mikono ya dora
baada ya wezi waliokuwa wakiiba kukamatwa na kumtaja yeye kuwa ndiye alikuwa
wakala mkubwa wa kununua vitu vya wizi ambapo alikamatwa mwaka huohuo wa 2000
na kupelekwa polisi ambako aliandaliwa mshitaka na kupelekwa mahabusu.
Baada ya
kupelekwa gerezani na kuwasimulia wenzake kilichompeleka humo alipata waalimu
ambao walimufundisha namna ya kuiba vitu vikubwa na namna gani ya kijihami na
kumshauri aachane na kununua vitu vya wizi.
Baada ya
kushawishiwa nililianza kufanya matukio mbalimbali ingawa ingawa sikuweza kukamatwa na kesi hizo,mfano
niliwahi kwenda kwenye duka la kituo cha mafuta na kumshawishi mlinzi aache
kazi na kwamba nitampeleka sehemu nyingine ili aweze kupata kazi nzuri.
Siku iliyofuata
nilienda kumtembelea mlinzi huyo na kumkuta amelala kesho yake tulienda na
wenzangu usiku tukafungua tukaiba simu zote,matukio yangu yalikuwa ya kwenda
kuwashawishi walinzi na kuwapa pesa ili sisi usiku tukaibe na kwa hili nataka
nikwambie hakuna mlinzi ambaye siyo mwizi.
Makuyu
anaeleza kuwa walipokuwa wakitoa vitu vya wizi mlinzi pia alikuwa akipata mgawo
wake na kwamba kitendo cha kufungua duka na kuhamisha bidhaa kilikuwa ni cha
muda mfupi sana.
Bidhaa
tulizokuwa tukiiba tulikuwa tukienda kuwauzia wenye maduka na pia fahamu kuwa
hata hawa wafanya biashara wa maduka ni wezi hili nalithibitisha hata kama
nikiambiwa kutoa ushuhuda nitatoa ndiyo maana tulikuwa hatupati shida ya kuuza
vitu vyetu vya wizi.
Makuyu
anasema akiwa gerezani alifanikiwa kudhaminiwa lakini licha ya kupata dhamana
hakuweza kukaa uraiani kwa amani kwani kila tukio baya la wizi lilipokuwa
likitokea polisi walienda kumkamata hali ambayo ilimyima amani.
Mnamo tarehe
26/12/2009 alimpiga mtu mmoja ambaye aliwahi kumtukana na kisha akakimbilia
Mwanza na kwamba siku hiyo walipokutana alimua kumpiga na mtu huyo alikwenda kuripoti kituo cha
polisi na kesho yake polisi walikwenda kumkamata na walipomfikisha kituoni kama kawaida yao walimbambikiza kesi ya
unyanga’nyi wa kutumia silaha na
kupatikana na bangi.
Niliendelea
na kesi hiyo ambayo ilikuwa chini ya hakimu Richard Maganga lakini baada ya
kuona haiendi vizuri niliandika barua ya kumtaka ajiondoe katika kesi hiyo
lakini alikataa na tarehe mwezi wa nane
mwaka 2010.
Anasema
ilipofika mwezi wa tisa tarehe 9 mwaka huohuo hakimu huyo alimufunga tena
kifungo cha miaka 30 jera na kuchapwa viboko 24 kwa kosa la unyanga’nyi hata
hivyo sikuridhika na hukumu hiyo ambapo nilikata rufaa ambayo ilinitoa mnamo
tarehe 31 mwezi wa tano mwaka huu.
Makuyu
anaeleza kuwa baada ya baada ya kuhukumiwa na Maganga alipelekwa katika gereza
la Butimba jijini Mwanza na kwamba akiwa huko alijifunza mambo mengi na aliona
mambo mwengi ambayo yalimusukuma kabisa kuacha wizi.
Kwakweli
baada ya kurudi niliamua kwenda polisi tarehe 21.8.2013 na kuonana na mkuu wa
upelelezi wa wilaya ambapo nilimuambia kuwa kuanzia sasa mimi ni raia mwema na
pia nimeamua kuwatafuta nyie waandishi ili mfikishe taarifa hizi kwa jamii kuwa
mimi siyo mwizi tena,
Niliamua
mwenyewe kwenda polisi kujisalimisha na kwa hili sina shaka maana naamini mungu
ananilinda maana hata kesi yangu nilishinda kwa nguvu zake maana hata wakili wa
serikali aliyekuwa ananitetea alisema hawahi kuona kesi kama yangu,yaani mtu
unafungwa mara mbili kwa mwezi mmoja.pasipo hata kujitetea.
Natoa wito
kwa vijana wa nchi hii wabadirike kama nilivyobadirika mimi nimejionea mambo
mengi gerezani,mfano vijana wa Musoma waache vikundi walivyonavyo kama vile
Jamaica mokazi,midomo ya furu na uchakavu na watambue kuwa gereza siyo mahali
pa kuishi na unapotoka gerezani hukai kwa amani kutokana na jamii kutokuamini.
Makuyu
anabainisha wenzake waliokuwa wakifanya nao kazi hiyo ambao wameshauwawa kuwa
ni pamoja na Sauri Magembe Bwire maalufu
kwa jina la Bebeto.Devis Manyama,Jumanne Mjungu na Stivin Wiliam ambao wote kwa
hivi sasa ni marehemu na walikufa kwa kupigwa na wananchi
Lakini pia anamuomba
rais Kikwete asitoe msamaha kwa wafungwa wa miaka mitano na kurudi chini kwani
hao wanakuwa hawajifunza kitu chochote na ndio maana wakiachiwa huanza tena
vitendo vya uharifu.
Huyo ndiye
Makuyu Magai aliyeamua kijisalimisha polisi baada ya kutoka gerezani.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment