NA BERENSI
ALIKADI,SIMIYU
MEI 22,2014,
Imeelezwa
kuwa wanawake tkribani 454 kati ya vizazi
100,000 hufa kila mwaka kutokana na uzazi.
Mganga mkuu
wa mkoa wa simiyu,Dr,Mageda Kihurya mjini Bariadi kwenye uzinduzi wa kampeni ya
uzazi wa mpango ngazi ya mkoa iliyojulikana kama nyota ya kijani.
Alisema
tafiti zinaonyesha kuwa upo uhusiano mkubwa
kati ya matumzi ya uzazi wa mpango na afya ya mama na mtoto na kwamba
matumizi haya yanawez kupunguza vifovitokanavyo na na uzazi kwa asilimia 44 na kupunguza vifo
vya kupungza vifo vya watoto kwa asilimia
10-12.
Dr Mageda
alisema hiyo ni kwa sababu ya uzazi wa
mpango humuwezesha mama kupumzika kati ya mimba moja hadi nyingine na pia
humsaidia mama kuepuka mimba zisizotarajiwa na hivyo kupunguza
tatizo la utoaji mimba holela
Aidha
alifafanua kuwa sense ya watu na makazi ya mwaka 2012 inaonyesha kuwa nchi yetu
ina idadi ya ya watu milioni 45 ikiwa ni
ongezeka la kasi,idadi isiyowiana na
ongezeko la pato la kiuchumi la nchi yetu hali inayotulazimu sisi sote kuongeza
juhudi katika kuwekeza kwenye huduma za jamii kama vile elimu na afya.
Kwa upande
wake mwakilishi wa shirika la misaada la Marekani USAID kupitia chuo kikuu cha John Hopkins,,Dr Rose Madida
aliwataka wanawake kuzaa kwa kufuata uzazi wa mpango na kuachana na mila potofu
kuwa kuzaa watoto wengi utajili.
Baadhi ya
wananchi wanaotumia uzazi wa mpango mkoani hapa wamelitoa ushuhuda wao na
kueleza kuwa uzazi wa mpango ni njia sahihi ya kumsaidia mtu kujua namna
atakavyoweza kuituza familia aliyonayo.
Akizindua
mpango huo mkuu wa mkoa wa Paschal Mabiti pamoja na kuupongeza mpango huo
ameziagiza halimashauri za wilaya mkoani humo kupanga bajeti kwa ajili ya
kuusaidia mpango huo na kwamba hata serikali kuu itahakikisha inafanya hivyo.
Uzinduzi huo
ulioenda sambamba na upimaji wa virusi,ufungaji wa uzazi na mafunzo ya uzazi
salama toka katika mashirika mbalimbali kama vile umati,Amreef na
Ingenderheath.
mwisho
No comments:
Post a Comment