
Tetemeko kubwa la ardhi limeipiga
Chile na kusababisha tishio la kutokea kwa tsunami, katika eneo lake la
pwani na maeneo mengine ya bahari ya Pacific.
Tetemeko hilo lenye
ukubwa wa 8.3 katika vipimo vya ritcha, lilipiga maeneo ya pwani na
kuenea kwa kilomita 250 kaskazini magharibi wa mji mkuu Santiago.Nchi hiyo imewahamisha wakazi milioni moja katika eneo la pwani, Rais wa Chile amethbitisha watu watano wamepoteza maisha baada ya tetemeko hilo kupiga
Kumeshuhudiwa matetemeko mingine midogomidogo katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment