Wednesday, September 16, 2015

Papa Francis kutembelea Kenya na Uganda


Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis atatembelea Kenya Novemba 25 kabla ya kuelekea Uganda siku mbili baadaye.
Papa Francis ashangiliwa na waumini Vatican.
Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis atatembelea Kenya Novemba 25 kabla ya kuelekea Uganda siku mbili baadaye na kisha Jamhuri ya Afrika ya Kati hapo tarehe 29 mwezi huo.
Mwezi Juni kiongozi huyo mzaliwa wa Argentina alieleza kikao cha makasisi kutoka kote ulimwenguni kuwa alikusudia kufanya ziara yake ya kwanza barani Afrika kwa kutembelea Kenya ingawaje ziara hiyo haikuwa imedhibitishwa wakati huo kutokana na matatizo ya kimipango.
Papa Francis hakufafanua matatizo hayo lakini alikuwa akizungumza miezi miwili baada ya kundi la wanamgambo  kutoka Somalia la Al-Shabaab kushambulia wakristo kwenye chuo kikuu karibu na mji wa Garissa ambapo wanafunzi 148 waliuwawa. Nchi ya Kenya imeshuhudia mashambulizi ya kigaidi ya mara kwa mara kutoka wanamgambo wa Al-Shaabab..
chanzo sauti ya amerika

No comments:

Post a Comment

Comments System

disqus

Disqus Shortname

msora

Popular Posts

Header Ads

ad