
Wanasiasa saba waandamizi
wamefurushwa kutoka kwa serikali ya muungano katika Jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo baada ya kumuandikia rais wakimtaka kutokwamilia
madaraka, kulingana na maafisa.
Katika barua kwa Joseph
Kabila,viongozi wa G7,kundi lenye vyama ndani ya muungano huo lilitaka
hatua kuchukuliwa ili kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika kufikia mwezi
Novemba.Mda wa kikatiba wa rais Kabila unakamilika mwaka ujao,lakini amekataa kuthibitisha kwamba hatowania muhula mwengine.
Upinzani pia unahofia kwamba uchaguzi huo utacheleweshwa.

Msemaji wa serikali Lambert Mende alikana kwamba bwana Kabila alitaka kukiuka katiba kulingana na n chombo cha habari cha Reuters.
CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment