Matokeo
ya ukaguzi wa kimatibabu uliofanyiwa mabaki ya mwili wa aliyekuwa rais
wa Burkina Faso marehemu Thomas Sankara miaka 28 baada ya
kuuawa,yanaonyesha kuwa mwili wake ulijaa risasi kulingana na wakili
aliyekuwa akiwakilisha familia yake kulingana na mtandao wa facebook wa
kituo cha habari cha Burkina 24.
Familia yake ilikuwa ikingojea
matokeo ya DNA kuthibitisha kwamba mabaki hayo yalikuwa ya bwana
Sankara,wakili Benewende Sankara aliviambia vyombo vya habari nchini
humo.
Mariam Sankara mkewe marehemu Thomas Sankara
Bwana Sankara aliuawa katika mazingira ya
kutatanisha akiwa na umri wa miaka 37 na kundi la wanajeshi mwezi Octoba
mwaka 1987,na alizikwa kwaa haraka kufuatia mpainduzi yalioongozwa na
mrithi wake Blaise Compaore.
No comments:
Post a Comment