SERIKALI YA CHINA IMESEMA IKO TAYARI KUWEKEZA KATIKA MKOA WA SIMIYU KWA KUJENGA VIWANDA MBALIMBALI VIKIWEMO VYA NGUO NA MAZIWA NA NYAMA KUTOKANA NA MKOA HUO KUONYESHA KUWA NA RASILIMALI NYINGI KAMA MIFUGO NA PIA NDIO UNAONGOZA KWA KUZALISHA ZAO LA PAMBA NCHINI,
AKIONGEA NA
VIONGOZI MBALIMBALI WA MKOA WA SIMIYU KUPITIA KWA MKALIMANI WAKE,YE TIANFA BALOZI MDOGO WA CHINA NCHINI TANZANIA,ZHANG
BIAO,AMESEMA NCHI YAKE IKO TAYARI
KUWEKEZA KATIKA VIWANDA KATIKA MKOA WA SIMIYU ILI KUUSADIA MKOA HUO KUKUA KIUCHUMI IKIWA NI
PAMOJA NA KUWAPA AJIRA VIJANA WA MKOA WA
SIMIYU.
KWA UPANDE
WAKE MKUU WA MKOA WA SIMIYU ANTHONY MTAKA AMEMUHAKIKISHIA BALOZI HUYO KUWA MKOA
WA SIMIYU UKO TAYARI KUWAPOKEA WAWEKEZAJI KUTOKA NCHINI CHINA WATAKAOHITAJI KUWEKEZA KATIKA MKOA WA SIMIYU
NA PIA WATAHAKIKISHA WANAWAPA USHIRIKINO WA KUTOSHA NA ULINZI PIA,,
BAADHI YA
WADAU WA MAENDELEO WA MKOA WA SIMIYU WAMESEMA UJIO WA BALOZI HUYO NI FARAJA
KWAO KWANI HUENDA UKAFUNGUA MILANGO NA FURSA KATIKA NYANJA MBALIMBALI ZA
KIUCHUMI KATIKA MKOA HUU
BALOZI HUYO
AMETEMBELEA MKOA WA SIMIYU IKIWA NI MWALIKO
WA MKUU WA MKOA WA SIMIYU AMBAPO BAADA YA KUONDOKA MKOANI SIMIYU AMEELEKEA
MKOANI MWANZA,
mwisho
No comments:
Post a Comment