Na Berensichina,sept
17,2017,ngombe 345 wapigwa mnada,
hakimu mkazi
mwandamizi mfawidhi wa mahakama ya mkoa wa simiyu john nkwabi ameamuru
kutaifishwa na kipigwa mnada jumla ya
ngombe 345 waliokamatwa wakichunga katika pori la akiba la maswa kinyume
cha sheria ya wanyamapori
akizungumza
mara baada ya kumalizika kwa mnada huo uliofanyika wilayani meatu meneja wa
pori la akiba la maswa lusato masinde amesema wameamua kuuza mifugo hiyo baada
ya mahakama kutoa amri kulingana na
sheria ya wanyama pori namba 5,2009 kifungu cha 111.
aidha meneja
huyo amewaonya wafugaji ambao watakaidi agizo la mhe.rais la kuondoa mifugo yao
kwa hiyari na kuacha kuchungia katika pori hilo
kwani msako wa kukamata mifugo hiyo ni endelevu na mifugo itakayokamatwa
itaendelea kutaifishwa kwa mjibu wa sheria
kwa upande
wake darali aliyesimamia zoezi la kuuza ngo’mbe hao kutoka kampuni ya abajaja
christopher kabenga amewataka wanunuzi wote kuhakikisha wanatembea na
stakabadhi halisi waliyopewa wakati watakapo kuwa wanasafirisha mifugo hiyo ili
kuepuka usumbufu njianii
No comments:
Post a Comment