KANISA LAMKANA MWALIMU ALIYEDAIWA KUBAKA MWANAFUNZI
NA Berensi Alikadi -Bunda.KANISA la Angilikana wilayani Bunda limemkana mwalimu mmoja aliyekuwa akifundisha shule mmoja wa awali ya Compassion alishitakiwa kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wake.
Akizungumza na Gazeti hili juzi ofsini kwake mkurugenzi wa huduma kituo cha huduma ya mtoto (TZ344) Ngai Emanuel alisema kuwa malimu huyo Amosi Julius ambaye hivi karibuni alifikishwa katika mahakama ya wilaya hiyo kwa shitaka la kubaka mwanafunzi siyo mwalimu wa kituo chao bali ni mwalimu wa shule ya awali ya kanisa la moja la warokole lilliloko mtaa wa Chiringe.
Alisema kuwa kitendo cha mwalimu huyo kudai mahakamani hapo kuwa ni mwalimu wa shule ya Compassion inayomilkiwa na kanisa hilo siyo ya kweli na kwamba hata wao kama kanisa wameshangaa sana kusikia taarifa hizo kwenye vyombo vya habari kuwa mwalimu huyo alidai kuwa yeye ni mwalimu wa shule ya kanisa hilo.
''Mimi nataka nikwambie mwandishi shirika hili la Compassion linafadhili makanisa mengi na wala siyo Angilikana pekee hivyo mimi nakuhakikishia kuwa mwalimu huyo sio wetu bali anafundisha katika shule ya kanisa la hapo chiringe hivyo sisi hatuhusiki kabisa na mwalimu huyo'' alisema mkurugenzi huyo kwa msisitizo.
Naye katibu wa jimbo hilo mkoani Mara Francis Senda alisema kuwa kitendo cha mwalimu huyo kusema uongo mahakamani si cha kiungwana na kwamba hata wao wanatarajia kumfungulia mashitaka mengine ya kulichafua kanisa hilo kwa kulisingizia uongo, ambapo pia aliwatahadhalisha wananchi kuhusu mwalimu huyo.
Mnamo october22 mwaka huu mwalimu huyo alifikishwa katika mahakama ya wilaya hiyo na kusomewa shitaka la kubaka mwanafunzi wa miaka 9 na mwendesha mashitaka wa polisi Hamza mdogwa, ambapo alikana kosa lake na kuomba dhamana alipoulizwa na hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya hiyo Joacimu Tiganga kuhusu kazi anayofanya ndipo alijibukuwa yeye ni mwalimu wa shule ya awali ya Compassion inayomilikiwa na kanisa Angilikana la mjini Bunda.jambo ambalo ni la uongo.
Hata hivyo mshitakiwa huyo hakupatikana tena kuhusu kutoa ufafanuzi wa kauli yake kutokana na kuwa yuko gerezani .
MWISHO
No comments:
Post a Comment