MWENDESHA BAISKELI AFA KWA KUGONGWA NA GARI
NA Berensi Alikadi-Bunda.MTU mmoja amekufa papo hapo baada ya kugongwa na gari dogo aina ya Noah lililokuwa likitoka mwanza kwenda mkoani Mara likisisafilisha maiti.
Polisi wilayani hapa wamethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo imetokea juzi majira ya saa sita mchanakatika kijiji cha Kunzugu nje kidogo mji wa Bunda na kulihusha gari hilo lenye namba za usajili T276BDF ambalo limugonga mwendesha baiskeli aliyefahamika kwa jina la Nchambi Doto 19 mkazi wa kijiji hicho cha kunzugu.
Imeelezwa ,kuwa gari hilo ambalo lilikuwa limebeba maiti toka jijini Mwanza na kuelekea Majita wilaya ya Musoma Vijijini lilipofika eneo hilo lilitaka kulipita gari jingine aina ya Toyota Land Cruser huku likiwa mwendo kasi na kumbe kwa mble yake alikuwepo mwendesha baiskeli huyo ndipo lilipomgonga na kufa papo hapo.
Kwa mjibu wa watu walioshuhudia ajali hiyo walisema kuwa gari hilo lilimgonga vibaya na kwamba alivuja damu nyingi kabla ya kifo chake kutokanana mwendo mkali lililokuwa nao licha ya kwamba lilikuwa limebeba maiti.
Akizungumza na gazeti hili baba mdogo wa Marehemu aitwaye Alphonce Migato alisema kuwa maiti ya ndugu yao huyo imehifadhiwa katika hosptali ya DDH Bunda ikisubili taraibu za mazishi zikiandaliwa.
Hata hivyo dereva wa gari hilo alifanikiwa kutoroka baada ya ajali hiyo ambapo gari hilo linashikiliwa katika kituo cha polisi Bunda na ndugu wa marehemu aliyekuwa akisafilishwa kwenda Musoma walitafuta gari jingine na kuweka maiti hiyo na kuendelea na safari.
Hiyo ni ajali ya pili kwa muda wiki moja kwa magari aina yaNoah kugonga na kuuwa ambapo wiki iliyopita mtu mmoja Makaba Lukas mkaziwa mtaa wa Manyamanyama kugongwa na gari aina ya Noah katika eneo la Manyamanyama,gari hilo lilikuwa litoka Musoma kwendawilayani Bunda
Wakati huo huo mtu mmoja aitwaye Mwita Marwa Machugu32 mkazi wa mtaa wa Nyamakokoto juzi alifikishwa katika mahakama ya wilaya ya Bunda akituhumiwa na shitaka la kumbaka Binti mdogo mwenye umri wa miaka 13 jina linahifdhiwa.
Mbele ya hakimu James Manota ilidaiwa na mwendesha mashitaka wa polisi Hamza Mdogwa kuwa mnamo November 3 mwaka huu majira ya saa kumi na mbili jioni huko katika mtaa wa Nyamakokoto mshitakiwa alimbaka mtoto huyo nyumbani kwake.
Ilielezwa mahakamani hapo kuwa siku ya tukio mshitakiwa huyo alimuta binti huyo nyumbani kwake na kuanza kumpa pombe ya Gongo na kwamba alipoona amelewa alimvutia chumbani kwake na kuanza kumbaka, hata hivyo baada ya kumaliza kumbaka alimuacha akaenda kwao baada ya kupata fahamu ndipo alipotoa taarifa kwa wakubwa wake ambao pia walitoa taarifa polisi.
Mshitakiwa huyo alikana shitaka hilo na kupelekwa rumande hadi 22Nov mwaka huu kesi yake itakapotajwa tena
No comments:
Post a Comment