Thursday, August 30, 2012

Michezo

Fulham yazikubali senti za Tottenham


Moussa Dembele
Mchezaji wa Ubelgiji Moussa Dembele kuichezea Tottenham
Klabu ya Tottenham imepata idhini ya kuendelea mbele na mipango yake ya kushauriana na kiungo cha kati wa klabu ya Fulham, Moussa Dembele, kufuatia vilabu hivyo kuafikiana juu ya malipo ya kumnunua mchezaji huyo.
Mchezaji huyo wa Ubelgiji yumo katika hali ya kuhudumu mwaka wake wa mwisho katika mkataba na timu hiyo ya Fulham inayochezea uwanja wa Craven Cottage, na hakushiriki katika mechi ya kombe la Capital One dhidi ya Sheffield Wednesday, wakati timu yake iliposhindwa.
Meneja wa Fulham, Martin Jol, amesema Dembele, mwenye umri wa miaka 25, yumo katika hali ya kupimwa hali yake ya afya katika klabu ya Tottenham.
Dembele aliingia Fulham kutoka klabu ya Uholanzi ya AZ Alkmaar, kwa gharama ya pauni milioni 5, mwaka 2010.
Hayo yakiendelea, Fulham imekuwa katika hali ya kushauriana na Kieran Richardson, baada ya kuelewana na Sunderland kuhusu kitita kinachohitajika kumpata mlinzi huyo.
Meneja wa Sunderland, Martin O'Neill alithibitisha kwamba tayari wamekubaliana juu ya kiwango cha pesa ambazo Fulham watatoa kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27.
Habari hii kwa hisani ya idhaa ya Kiswahili ya BBC 

No comments:

Post a Comment

Comments System

disqus

Disqus Shortname

msora

Popular Posts

Header Ads

ad