Serikali ya Syria inatumia mabavu' asema Morsi

Rais Mohammed Morsi
Rais wa Misri, Mohammed Morsi, ameikashifu serikali ya Syria na kusema kuwa inatumia mabavu.
Rais Morsi aliyasema hayo katika hotuba yake nchini Iran ambayo ni mshirika mkubwa wa Syria.Morsi alisema kuwa ni wajibu wa kila mtu kuunga mkono upinzani nchini Syria ili uungane dhidi ya kile alichokitaja kama utawala wa kimabavu.
Katika hotuba yake katika mkutano maalum mjini Tehran, bwana Morsi alisema kuwa ni jukumu lao kimaadili kuunga mkono upinzani nchini Syria sawa na kuwa mkakati sawa wa kisiasa
Waziri wa mambo ya nje wa Syria, Walid Mouallem, alisema kuwa wajumbe wa Syria waliondoka kwenye mkutano huo wakati wa hotuba ya rais Morsi, ambayo aliitaja kama ya uchochezi wa kuendelea kumwaga damu ya wanachi wa Syria.
Ziara ya rais Morsini ya kwanza ya afisaa mkuu wa Misri, tangu mapinduzi ya kiisilamu mwaka 1979.
No comments:
Post a Comment