Na Berensi Alikadi-Bunda.
BAADA ya watu wasiofahamika kuchoma mabweni mawili ya kidato cha pili katika sekondari ya Ikizu iliyoko wilayani Bunda mkoani Mara inayomilikiwa na kanisa la Kisabato ,shirika lisilo la kiserikali la ADRA la mkoani Arusha limetoa msaada wa vitu mbalimbali ili kusaidia wanafunzi waliounguliwa na vitu vyao.
Akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo kabla ya kukabidhi vifaa hivyo,mwenyekiti ya kanisa hilo jimbo la Mara mchungaji Daudi Makoye alisema kuwa shirika hilo limetoa vifaa hivyo baada ya kupata taarifa ya kuchomwa kwa mabweni hali ambayo imesababisha wanafunzi kukosa mahali pa kulala na kukosa vifaa muhimu zikiwemo nguo,magodoro na madftari yao.
Mwenyekiti alivitaja vifaa hivyo vilivyotolewa kuwa ni masweta122,suruali 94,mashati mashati 82 ,blanket 83,matandiko 94 na majaketi42 vyote vikiwa na thamani ya shilingi million 3,736,000.ambapo alisema kuwa wanatarajia kupata misaada mingine toka kwa wananchi wenye mapenzi mema hususa ni viongozi wa serikali ambao walisoma katika shule hiyo.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa wanafunzi hao mkuu wa wilaya hiyo Joshua Mirumbe alilipongeza shirika hilo kwa mchango wake mkubwa lililotoa kwa kanisa hilo wa kutoa vifaa hivyo ambapo aliyataka mashirika mengine pia kuiga mfano wa shirika hilo.
Mirumbe ambaye pia alisoma katika shule hiyo alisema kuwa shirika hilo limekuwa likichangia katika miradi mbalimbali ya maendeleo katika nchi mbalimbali za afrika na kwamba mchango wake huo iliotoa utasaidia wanafunzi hao ambao vifaa vyao viliungulia kwenye mabweni hayo.
Aidha mkuu huyo aliwapongeza wanafunzi waliopatwa na mkasa huo kwa kuonyesha moyo wa uvumilivu wa kuendelea na masomo ambapo amewaomba waendelee kusoma kwa bidii na kujiandaa na mitihani wakati ambapo serikali ya wilaya na mkoa vikiendelea kutafuta misaada mbalimbali kwa ajili yao.
‘’Napenda niwafahamishe kuwa sisi kama wilaya tunaendelea kuomba misaada mbalimbali toka kwa wananchi na mashirika tumeshayaomba mashirika yanayonunua pamba hapa kwetu kama vile kampuni ya Mathayo, Badugu,Olam, Aliance na Bulamba Ginery ili waweze kutusaidia na michango hiyo ikija tutaiwasilisha hapa tuwape ‘’alisema Mirumbe.
Alitumia pia fursa hiyo kuwaambia wanafunzi hao kuwa tume aliyoiunda bado inaendelea na kazi na kwamba itakapomaliza kazi yake itatoa taarifa kuhusiana na tukio hilo ambalo linahusishwa na mlipuko na wala siyo umeme kama ambavyo imekuwa ikidaiwa na baadhi ya watu.
Mwisho
No comments:
Post a Comment