
Wanajeshi wa Kenya
nchini Somalia
Ujumbe wa Umoja wa Afrika wa
kudumisha amani nchini Somalia AMISOM, unasema utachunguza tuhuma kuwa
wanajeshi wa Kenya waliwaia kwa kuwapiga risasi raia 7 wa Somalia wakati
wa makabiliano na wapiganajai wa Al shabaab hapo jana Jumapili.
Wanajeshi hao inasemekana waliwaua raia saba
katika kijiji cha Janaay Cabdalla wakati mapigano yalipotokea umbali wa
kilomita 50 kutoka mji wa Kismaayo.Msemaji wa AMISOM kanali Adi Aden amesema wakati ukweli wa kesi hiyo utakapojulikana watachukua hatua.
Msemaji huyo aliambia BBC kuwa wanajeshi wa Kenya waliwafyatulia risasi wanaume hao waliokuwa wameketi nje ya duka moja katika kijiji cha Janaay Cabdalla.
Wanajeshi wa Kenya na wale wa Somalia awali walivamiwa na wapiganaji wa Al Shebaab huku ripoti zikisema kuwa pande hizo mbili, zilipata majeruhi.
Kwa mujibu wa msemaji huyo, wanakijiji waliouawa ambao ni wanaume saba hawakuwa wanamgambo bali raia wa kawaida.
Duru zinasema kuwa wanaume hao walikuwa wamepiga foleni kununua sukari.Aidha msemaji wa jeshi la Muungano wa Afrika nchini Somalia, (AMISOM) alisema kuwa hawezi kuthibitisha tukio hilo, lakini madai hayo yatachunguzwa.
Wanajeshi wa Somalia wakiungwa mkono na wale wa Uganda na Kenya pamoja na vikosi vingine kutoka nchi tofauti za Afrika, wanakaribia kuuzingira mji wa Kismayo,na ili waweze kufanikiwa katika kuuteka mjihuo, wanachi wa pale watahitaji kushirikiana nao.
Wanajeshi wa Kenya wamewahi kutuhumiwa kwa kuwaua raia wakati wakifanya mashambulizi katika maeneo ya Al Shabaab .
Shirika la kuwahudumia wakimbizi UNHCR linakadiria takriban wakimbizi 10,000 wameutoroka mji wa Kismayo katika kipindi cha wiki moja iliyopita.
No comments:
Post a Comment