Friday, September 28, 2012

Majeshi ya Amisom yauteka mji wa Kisimayo

Majeshi Kismayo
Hatimaye wanajeshi wa AMISOM wameuteka mji wa Kismayo.
Msemaji wa jeshi la Kenya Kanali Cyrus Oguna aliambia BBC kuwa wanajeshi wa Kenya kwa ushirikiano na wale wa Somalia walianza harakati zao mapema asubuhi ya leo.
Kwa sasa wanajeshi wa AMISOM wanaendelea na harakati zao kuingia ndani kabisa ya mjini huo. Kamanda wa majeshi hayo Luteni Generali Andrew Gutti, amesema AMISOM imewataka wenyeji wa mji wa Kismayo kuwa watulivu.
Kwenye taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, Luteni Generali Gutti alisema kuwa nia na lengo la wanajeshi hao ni kuwakomboa watu wa Kismayo na kuwawezesha kuishi kwa amani na usalama.
Alidokeza kuwa harakati zinaendelea kulenga maeneo ya Al Shabaab mjini humo.
Aliongeza kuwa angewataka wapiganaji waliosalia Kismayo kujisalimisha
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baadhi ya wapiganaji wa kundi hilo walio mjini humo, wameelezea nia yao kutaka kujisalimisha. Nayo AMISOM imewahikikishia usalama wao ikiwa wataweza kujisalimisha
Lakini mwandishi wa BBC anasema kuwa Al Shabaab husalimu amri kwa muda wakati wanapokabiliwa na majeshi yenye nguvu kuwaliko.
Ndege za kivita za Kenya zilifanya mashambulizi ya angani mapema wiki hii na kuharibu bohari lenye silaha za wapiganaji hao mjini humo.
Wiki iliyopita, Al Shabaab walijiandaa kuondoka Kismayo na hata kuwahamisha wapiganaji wao pamoja na silaha.
Mji huo wa bandarini ni muhimu kwa Al Shabaab kwani wanautumia kuingizia silaha na pia kuwatoza kodi wenyeji wa mji huo.
Hatua ya wao kupoteza mji huo, itakuwa ni pigo kubwa kwao, lakini wapiganaji hao wa Al Shabaab bado wana uwezo wa kufanya mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa Somalia na wale wa Muungano wa Afrika hata katika sahamu ambazo wanajeshi hao wanadhibiti.
Chanzo BBC

No comments:

Post a Comment

Comments System

disqus

Disqus Shortname

msora

Popular Posts

Header Ads

ad