NA Berensi Alikadi-Bunda
IMEELEZWA Kuwa
njia pekee ya kumsaidia mtoto wa kike ni kumpa elimu bora itakayomsaidia
katika maisha yake ya baadaye na wala sivinginevyo.
Kauri hiyo imetolewa jana
mjini Bunda na mbunge wa viti maalumu kundi la vijana wa chama cha mapinduzi
mkoa wa Mara Ester Bulaya wakati
alipokuwa akiongea na wazazi na wanafunzi kwenye mahafali ya kwanza ya shule ya
waschana ya Mkwezi iliyopo mjini Bunda.
Alisema kuwa mtoto wa kike
anayonafasi kubwa ya kufanya vizuri kielimu kama
ataendelezwa ipasavyo na kwamba ile dhana ya kumbeza mtoto wa kike kwa kutompa
elimu sasa imepitwa na wakati.
Mbunge huyo aliwataka wazazi
wa watoto hao waliohitimu kidato cha nne kuwasadia zaidi watoto hao ili waweze
kuendelea na masomo ya vidato vya juu ambayo yawasaidia kuingia katika soko la
ajira hapa nchini na nje ya nchi.
‘’Ndugu zangu wazazi watoto
hawa sasa ndio wameanza hatua kubwa maana hii hatua waliyomaliza naweza kusema
ni kama nusu hivyo wasaidieni ili waweze kufikia malengo ya maisha yao nina imani wanandoto
nzuri ya kufika kileleni sasa tuwawezeshe ili wafaulu.’’alisema Bulaya.
Mbunge huyo alikubali
kumsomesha mwanafunzi Penina Wayoga hadi kidato cha sita baada ya kupata vyeti
sita ambavyo amefanya vizuri katika masomo ya hesabu,Fizikia,Sayansi uraia
Jografia na bailogia ambapo aliibuka kidedea kwa kupewa vyeti sita.
Awali wakisoma risala ya
kuhitimu masomo yao wanafunzi hao walisema kuwa walianza masomo shuleni hapo mwaka 2009 wakiwa wanafunzi 24 na sasa
wamehitimu wakiwa 41 ambapo sanaa
wanafunzi 20na sayansi ni wanafunzi 21.
Walisema kwa muda wote
waliosoma shuleni hapo wameweza kupata mafanikio mbalimbali ikiwa ni pamoja na
shule hiyo kushika nafasi ya 4 kati ya shule 29 kimkoa,na shule kushika nafasi
ya 36 kati ya shule 432 kikanda ambapo pia katika mtihani wa utimilifu
walishika nafasi ya kumi kati ya shule 164 kimkoa.
Wanafunzi hao walibainisha
kuwa pamoja na mafanikio hayo shule hiyo pia inakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo ukosefu wa maktaba,maabara jambo ambalo limechangia kudumaa
kwa maendeleo ya elimu shuleni hapo.
Akisoma risala ya shule hiyo
mkuu wa shule hiyo,Mwalimu Goodluck Muyenjwa alisema kuwa pamoja na shule hiyo
kufanya vizuri lakini bado lipo tatizo la wazazi kutolipa ada kwa wakati jambo
ambalo limesababisha uongozi wa shule hiyo kuwatowalipa watumishi mishahara kwa
wakati.
Muyenjwa alisema kuwa shule
hiyo pia inakabiliwa na tatizo la ukosefu wa umeme jambo limewafanya wanafunzi
wa shule hiyo washindwe kujisomea ipasavyo na kumuomba mbunge huyo aweze
kulifikisha kwa wahusika ombi ambalo alilikubali.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment