KAMATI ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Bunda imesitisha kwa muda malipo ya jumla ya shilingi 1.2 zilikuwa zilipwe kwa wananchi wa kitongoji cha Kirumi ambao wanatakiwa kupisha eneo ilo kwa ajili ya shughuli za uwekezaji za EPZA baada ya kubaini kuwa kulikuwa na majina hewa yaliyotakiwa kulipwa.
Mwenyakiti wa kamati hiyo ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo Joshua Mirumbe alisema jana ofisini kwakwe kuwa serikali hivi karibuni imeleta kiasi cha shilingi bilioni 1.2 kwa ajili ya kuwalipa wananchi ambao wanatakiwa kuhama eneo hilo lakini imegundulika kuwa kuna mchezo mchafu ambao ulikuwa umeshaandaliwa na baadhi ya wajanja katika halimashauri hiyo ili waweze kuhujumu malipo hayo.
Mirumbe alisema kuwa wakati pesa hizo zinaletwa kulikuwa na zoezi la sensa ya watu na makazi na pia wilaya ilikuwa ina maandalizi ya kupokea mwenge wa uhuru hivyo kamati ya ulinzi na usalama hakuweza kupata nafasi ya kuhakiki majina ya watu wanaostahili kulipwa kama kweli ni wenyewe ama laa.
Alisema kuwa wakati bado kamati ya ulinzi na usalama inajipanga alishangaa kuona halimashauri ya wilaya imeshaanza kuwalipa wananchi wa kitongoji hicho pasipo mpangilio jambo alilosema kuwa lingeweza kuleta manung’uniko makubwa kwa wananchi wengine.
‘’Tumepata taarifa ya kuwepo kwa majina hewa ambayo pia yalijiandikisha kuwa yanaishi katika kijiji hicho cha Tairo,kitongoji cha Kirumi wakati ni uongo watu hao wanaishi hapa mjini sasa mimi nasema hii ni pesa ya serikali lazima niisimamie atakayebainika amefoji jina atashughulikiwa kwa mjibu wa sheria nataka wote waelewe hivyo na kwa hilo stakuwa na mzaha’’alisema Mirumbe kwa msisitizo.
Alifafanua kuwa baada ya ofisi yake kupata taarifa ya kuwepo kwa majina hewa tayari ameunda tume ya kuhakiki majina hayo na kwamba kazi hiyo inaendelea vizuri na pindi itakapokamilika wale wanaostahili kulipwa watalipwa haki zao.
Hata hivyo amewataka wale wote watakaokuwa wamelipwa pesa zao wahakikishe wanahama na kuachia eneo hilo na watafute maeneo mengine ya kuishi ili liweze kuanza kufanyiwa maandalizi na wahusika.
MWISHO
No comments:
Post a Comment