NA Berensi Alikadi-Bunda.
JUMLA ya wanafunzi 10777 wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba mwaka huu 2012 katika wilaya ya Bunda.utakaofanyika kesho nchini kote
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana,afisa elimu ya msingi wa wilaya hiyo Labani Bituro alisema kuwa kati ya wanafunzi hao wavulana ni 5452 na wasichana ni 5325.tofauti na mwaka jana ambapo wanafunzi 12931 walifanya mtihani huo
Alisema wanafunzi hao wanatarajia kufanya mtihani huo katika shule 155 ambazo ni za serikali na shule 151 ni za watu binafsi na kwamba maandalizi yote yameshakamilika ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa wasimamizi watakaosimamia mtihani huo.
Bituro alisema kuwa wilaya hiyo imeandaa vituo 478 katika majimbo yote ya Mwibara na Bunda ambako mitihani hiyo itafanyika na kwamba maandalizi yamekamilika kwa asilimia mia moja.
Alifafanua kuwa wilaya imejiandaa ipasavyo kuhakikisha kuwa mtihanai huo utafanyika kwa amani na utulivu na kwamba wasimamizi wote wamekula kiapo na kwamba yeyote atakayekiuka kiapo alichokula na kuvujisha mtihani kwa kupewa hongo atachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kupelekwa mahakamani.
Afisa elimu huyo aliwataka wale wote waliochaguliwa kusimamia mtihani huo kuwa waaminifu na kuifanya kazi hiyo kwa kufuata maadili na uangalifu mkubwa kama walivyokula kiapo ili kuileta heshima wilaya hiyo.
''Tumewapa mafunzo ya kutosha na wamekula kiapo na kwa sababu ni waalimu wana dhamana ya serikali nina imanai kuwa wataifanya kazi hiyo vizuri lakini pia kwa yule atakayejichanganya akadanayika na vipesa akatoa majibu huyo kazi ni kwake maana hatutamuonea aibu naomba watambue hilo''alisema Bituro.
Nao baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali za wilaya hiii ambao wamehojiwa na gazeti hili kwa nyakati tofauti wamesema kuwa wamejiandaa ipasavyo katika kukabiliana na mtihanai huo wa darasa la saba ambapo wengi wao walionyesha kujiandaa ipasavyo.
''Kwakweli tumejiandaa vizuri sana kutokana na maandalizi na masomo tulivyofundishwa na waalimu wetu tuna imanai kuwa tutafanya mtihanai huo kwa ufanisi zaidi na tuna imani kuwa mungu atatusaidia''walisema wanafunzi wa shule ya msingi Kabalimu iliyoko katika mamlaka ya mji mdogo wa Bunda.
Mwisho
No comments:
Post a Comment