NA Berensi Alikadi-Bunda.
IMEELEZWA kuwa
ukosefu wa mitaji kwa wakulima ,usimamizi imara wa watalaam na utashi wa
kisiasa vimekuwa vikichangia kushuka kwa uzalishaji wa zao la pamba wilayani
Bunda kila mwaka.
Hayo yamesemwa jana na washiriki wa mkutano wa kuboresha
kilimo cha pamba katika wilaya hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Serengeti
Resort chini ya uneyekiti wa mkuu wa wilaya hiyo Joshua Mirumbe.
Wakichangia mada katika mkutano huo baadhi ya wadau na
wakulima wa zao hilo wamedai wakulima wengi
hawana mitaji ya kuendeleza zao hilo
na kwamba wengi wao wakishauza pamba hutumia pesa na kuzimaliza anbapo wengi
wao hukosa hata pesa ya kununua pembejeo za msimu ujao.
Mkaguzi wa bodi ya pamba katika wilaya za Bunda na
Serengeti,Igoro Maronga alisema kuwa suala la kilimo cha pamba sasa hivi
kimekosa usimamizi kuanzia kwa maafisa ugani hadi kwa wanasiasa ambao pia
wamekuwa halitilii maanani sana
licha ya kufahamu kuwa ndilo zao pekee linalowapa tija wapiga kura wao.
Igoro alibainisha kuwa
ukiukwaji wa masharti ya kanuni
kumi za kilimo cha zao hilo ,mbegu
kutochanganywa vizuri viwandani na kutoweka mbolea za samadi mashambani
kimekuwa chanzo kikubwa cha wakulima kupata mazao hafifu.
Naye Daudi Iramba afisa kilimo wa kata ya Hunyari alisema
kuwa kumekuwepo na tabia ya baadhi ya makampuni kuunda vikundi vya wakulima
vijijini bila kuwahusisha wataalam jambo ambalo limkuwa likiwapa shida maafisa
ugani walioko vijijini katika kufanya kazi
na vikundi hivyo.
Akizugumza kwa niaba ya wakulima wa pamba,mkulima mmoja
aliyejitambulisha kwa jina la Mayaya alisema kuwa dawa nyingi wanazopelekewa
wakulima kwa ajili ya zao hilo ni zile ambazo hazina ubora na kwamba yapo
makampuni kama vile Olam,Alliance zilichangia pia mazao kuharibika na kwamba ni
vema serikali ikariangalia hilo kwa upana zaidi.
‘’Changamoto kubwa inayotukabiri sisi licha ya hayo ni
pamoja na wakulima kuchanganya mazao na ni vema wakulima wakawa wanapatiwa
mafunzo ya mara kwa mara ili waweze kuwa na elimu ya kutosha maana hata hawa
maafisa ugani wengine hawawafikii wakulima ipasaavyo’’alisema mkulima huyo.
Akifungua mkutano huo wa siku moja mkuu wa wilaya hiyo
Joshua Mirumbe alisema lengo la mkutano
huo ni kuweka mkakati wa pamoja wa kuboresha zao la pamba ambalo ndilo
zao la biashara kwa wilaya hiyo ambapo hivi sasa uzalishaji wake unashuka kila
mwaka .
Mirumbe alisema kuwa kazi ya watumishi yaani maafisa
ugani,makampuni ni kutoa elimu kwa wakulima kuhusu kilimo cha kisasa cha zao
hilo na kwamba ndiyo maana ameitisha mkutano huo ili aweze kuwakutanisha wadau
wa kilimo,wakulima na watalam kwa ajili ya kuweka mkakati wa pamoja.
Alisema kuwa katika msimu wa mwaka huu wilaya hiyo ilikuwa
ikusanye kilo million 10 lakini kutokana
na ugonjwa ulizikumba kata za igundu na Namhura wilaya imefanikiwa kukusanya
hadi sasa jumala ya kilo million 8 na kwamba huenda hali ikapamba kutokana na
kwamba msimu bado unaendelea.
Mkutano huo umeshirikisha wadau wa kilimo, wakulima bora,
maafisa ugani,wawakilishi wa makampuni,maafisa tarafa watendaji wa kata na
waandishi wa habari.
Mwisho
No comments:
Post a Comment