NA Mwandishi
wetu Rorya.
21/8/2013
MKURUGENZI
wa halimashauri ya wilaya ya Rorya mkoani Mara,Ephraem,Nguyaine amewaambia
madiwani wa halimashauri hiyo kuwa kiasi cha shilingi million 14 zilizotumika
kutengeneza gari la halimashauri hiyo analotumia ni pesa ndogo sana sawa na
vijisent tu
Mkurugenzi
huyo alitoa kauri hiyo juzi agost 13/2013 kwenye kikao cha baraza la madiwani
hao lilifanyika katika wa Soa katika mji mdogo wa utegi.
Alisema kuwa
anashangazwa na madiwani wanaodai kuwa pesa hizo ni nyingi zilizotumika katika
matengenezo ya gari hilo lenye namba za usajili STK 5982 aina ya Toyota Land
Cruser V8
‘’Mimi
nawashangaa sana madiwani mnashangaa gari hilo kutengenezwa kwa gharama hiyo
mbona wenzetu Tarime la kwao walitengeneza kwa million 70 na lile la mkuu wa
mkoa lilitengenezwa kwa million 80’’alisema mkurugenzi huyo kwa dhihaka.
Hata hivyo
kauri hiyo ya mkurugenzi huyo ilipingwa vikali na madiwani hao ambao walisema
kuwa pesa hizo ni nyingi mno zilizotumika ukilinganisha na mahitaji ya
halimashauri hiyo.
Diwani wa
kata ya Mkoma kwa tiketi ya chadema,Lazaro Kitori alisema kuwa gari hilo pamoja
na kutengezwa kwa gharama hiyo lakini lilifanya kazi kwa muda wa miezi sita tu
na sasa limeharibika tena na kwamba huenda likahitaji pesa nyingi zaidi ya
hizo.
Hoja hiyo
iliungwa mkono na diwani wa kata ya Ikoma kwa tiketi ya chama cha mapinduzi
ambaye pia aliunga mkono na kutaka gari hilo liuzwe kwani ni la anasa na
linaitia hasara halimashauri hiyo ambayo bado ni change kimapato.
‘’Mwenyekiti
mimi nashangaa sana mkurugenzi huyu anajibu majibu kirahisi hatuwezi
kujilinganisha na wilaya za Tarime wala
na ofsi ya mkuu wa mkoa wenzetu wana mafungu ya kutosha kwakweli hili gari
tuliuze tununue angalau tipa liwe linasomba mchanga katika shule zetu badala ya
kuwa na gari ambalo ni la anasa’’alisema diwani huyo.
Hata hivyo
baadhi ya wananchi wa wilaya hiyo waliohojiwa na gazeti hili kuhusiana na suala
hilo wamedai kushangazwa na kauri ya kibabe ya mkurugenzi huyo kwani walidai
kuwa halimashauri hiyo inakabiliwa matatizo mengi ukiwemo ukosefu wa huduma
mbalimbali kwenye kata za halimashauri hiyo lakini mkurugenzi huyo halioni hilo
bali anatumia pesa nyingi katika kutengeneza gari analotumia yeye.
‘’Huyu
mkurugenzi wetu kwanza hana mahusiano na wananchi na muda mwingi jioni utamuona
akiwa na gari hilo kwenye mabaa na sasa kama kweli madiwani wameona halina
faidia ni bora liuzwe ili hizo pesa tujengewe hata zahanati na yeye anunuliwe
gari ambalo siyo la anasa.’’alisema John Omondi mkazi wa Utegi
Katika hatua
nyingine diwani wa tarafa ya Nyancha viti maalumu CCM,Pendo Odele amedai kuwa
halimashauri hiyo imegawa kiasi cha shilingi milioni 400 kwa upendeleo katika
kata nne huku zingine zikiachwa.
Diwani huyo
alisema kuwa pesa hizo ambazo zilitolewa kwa ajili ya kujenga hostel katika
shule mbalimbali za sekondari zilitolewa kinyemela kwani hazikupitia kwenye
kamati ya fedha mipango na utawala lakini zoezi hilo lilifanywa na mkurugenzi
na mwenyekiti wa halimashauri hiyo,Charles Ochere.
Alizitaja
kata zilipewa pesa hizo kuwa ni kata ya Roche ambayo inaongozwa na mwenyekiti
huyo ambayo ilipewa shilingi milioni mia moja,kata ya Labour ilipewa milioni
mia moja,kata ya Kisumwa ilipewa milioni mia moja,kata ya Kigunga ilipewa
million sabini na kata ya Thai ilipewa milioni therethini na kwamba pesa hizo
zilitolewa mwezi wa nne mwaka huu.
Hata hivyo
mwenyekiti wa halimashauri hiyo alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu pesa hizo
pamoja na mkurugenzi wake hawakuweza kutoa majibu ya kulidhisha na kufauati
hali hiyo madiwani wa kata 16 wameibuka na malalamiko hayo na kutaka wapewe
majibu sahihi katika kikao kijacho.
Siku za hivi
karibuni halimashauri ya wilaya ya Rorya imekuwa katika kashifa ya matumizi
mabaya ya pesa za serikali hususani katika ujenzi wa nyumba za halimashauri
hiyo