DIWANI WA CHADEMA AFICHUA NJAMA ZA CCM TARIME.
NA Berensi
Alikadi-Tarime.
5/8/2013
Diwani wa
kata ya Turwa katika halimashauri ya mji wa Tarime kupitia chama cha demokrasia
na maendeleo [Chadema] Charles Ndessi Mbusiro amesema chama cha mapinduzi CCM wilayani
Tarime kimepora uwanja wa michezo pasipo ridhaa ya wananchi.
Diwani huyo
alitoa tuhuma hizo juzi julai 28 mwaka huu wakati alipokuwa akihutubia maelfu
ya wananchi wa Tarime waliohudhulia maadhimisho ya miaka mitano tangia kifo cha
aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema marehemu Chacha
Zakayo Wangwe maadhimisho yaliyofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Serengeti.
Amesema kuwa
uwanja huo ni mali ya wananchi wote wa Tarime lakini chama cha mapinduzi kwa
hila zake baada ya kuona uwanja huo ukitumiwa mara kwa mara na Chadema katika
mikutano yake wamefanya ujanja na kupata hadi ambapo sasa wanadai kuwa ni mali
yao.
‘’Ndugu
zangu wananchi wa Tarime napenda kuwafahamisha kuwa uwanja huu mliopo sasa CCM
wamefanya njama na wameuchukuwa na wanadai kuwa ni wakwao na tayari wanataka
kujenga vibanda na wameshagawana vibanda kila kioongozi ana milango yake sijui
kama wananchi mnalijua hilo’’alisema diwani huyo huku akijibiwa na wananchi
kuwa hatujui na tunataka waurudishe.
Diwani huyo
ambaye pia ni mwenyekiti wa madiwani wa Chadema wilaya ya Tarime alidai kuwa
uwanja huo ulijengwa na wananchi wote kipindi cha mfumo wa chama kimoja na
kwamba CCM haina hati miliki wala haina mamlaka ya kupora kiwanja hicho ambapo
amesema wakiongoza halimashauri CCM wajuwe kuwa kiwanja hicho kitarudi mikononi
mwa wananchi na wala si vinginevyo hayuko tayari kuona nguvu za wananchi
zinaporwa na kundi la watu wachache.
Alifafanua
kuwa tayari wanataka ccm iwambie kama ni chama cha biashara ama ni chama cha
siasa kwani viongozi wa chama hicho ndio waliojipanga kufanya biashara katika uwanja
huo na kwamba hata kodi wanazokusanya sasa hivi kwa wamachinga ni za kuwaibiwa
wananchi hivyo Chadema haitakuwa na mzaha katika hilo ni lazima kitaeleweka.
Diwani huyo
alieleza kuwa kitendo cha chama hicho kupora kiwanja hicho huku wakijua kuwa
siyo mali yao kinaonyesha dhahiri njisi kisivyowatakia mema wananchi wake na
kwamba kitendo hicho lazima kilaaniwe na kila mwananchi wa Tarime mpenda
maendeleo.
Wakiongea na
gazeti hili kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi wa mji wa Tarime wamedai
kusikitishwa na kitendo hicho ambacho walisema ni cha kifisadi na kwamba jambo
hilo si la kufumbia macho.
‘’Unajuwa
hawa watu wa magamba wamezoea sana
dhuruma na ufisadi hiki kiwanja ni cha wananchi wote na wala si cha CCM sasa
leo nimeshangaa kusikia kuwa wamekichukuwa kwa nguvu ili kiwe mali yao kwakweli
hili halitawezekana tumechoka kuonewa liwalo na liwe lazima wakirudishe’’alisema
mwananchi mmoja Mwita Mseti mkazi wa mtaa wa
rebu.
Kufuatia
tuhuma hizo gazeti hili lilimtafuta katibu wa chama hicho wilaya,ili aweze
kujibu tuhuma hizi lakini hakuweza kupatikana na wala mwenyekiti wake pia
hakuweza kupatikana.
mwisho
No comments:
Post a Comment