NA Berensi
Alikadi,Bunda.
5/8/2013
WATU wawili
wamefariki dunia juzi wilayani Bunda mkoani Mara katika matukio mawili tofauti
likiwemo la mme kuuwa mke wake na kisha yeye pia kuuwawa.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo lililotokea agost
2mwaka huu afisa mtendaji wa kata ya Mcharo Waziri kingialimtaja mwanamke mmoja
aliyekuwa akifahamika kwa jina la Pamera Samson mkazi wa kijiji cha Kisangwa
wilayani hapa alifariki dunia baada ya kunyongwa na mme wake.
Mashuhuda wa
tukio hilo wameliambia Tanzania daima kuwa mwanamke huyo ambaye kwa sasa ni
marehemu alikuwa ametengana na mme wake kutokana na matatizo ya ugomvi miezi
miwili iliyopita na kwamba mme wake huyo aliyekuwa akifahamika kwa jina la
Bature Masanja alikuwa amehamia katika kijiji cha Maliwanda kilichopo katika
wilaya hiyo.
Imeelezwa
kuwa siku ya tukio kulikuwa na sherehe nyumbani kwao na mwanamke ya kufungua nyumba na kwamba mme
wake huyo pia alifika hapo na kwamba wakiwa wanasherekea ndipo majira ya usiku
alipomuomba mke wake watoke waende sehemu kwa madai kuwa alikuwa na mazungumzo
naye.
Mashuhuda
hao walifafanua kuwa baada ya kutoka naye walienda mbali kidogo na hapo
nyumbani kwao na kwamba alipofika umbali fulani alimkamata mke wake wake huyo
na kumbaka ambapo baadaye alimaliza akamnyonga.
‘’Jana yake
asubuhi ndio mwili wake huyo mama ulionekana baada ya watu waliokuwa wakienda
shambani kuukuta na ndipo walipotoa taarifa hizo lakini kwa kuwa watu walimuona
anaondoka na huyo mme wake na kwa vile hakuweza kurudi tena pale ukweni kwakwe
waliamini kuwa ndiye aliyefanya tukio hilo’’alisema mwalimu mmoja wa shule ya
msingi Kisangwa ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini.
Alifafanua
kuwa baada ya taarifa hizo kuenea kijijini hapo walipiga yowe na kuanza kumsaka
mme wake huyo na ndipo walipompata akiwa amejificha mlimani nyuma ya shule ya
msingi Sengerema na kwamba baada ya kukamatwa alikiri kuwa ndiye aliyemuua mke
wake.
Kufuatia
hali hiyo wananchi walishikwa na hasira na ndipo walipoanza kumpiga na
kumkatakata kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake pasipo huruma hadi
alipokata roho.
Polisi
wilayani hapa waliweza kufika eneo la tukio na kukuta mtu huyo akiwa tayari
ameshakufa ambapo wariruhusu mwili huo uzikwe na ule wa mke wake pia na kwamba
hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa kutokana na tukio hilo.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment