Sunday, September 1, 2013

KAMUAHANDA, DAMU YA MWANGOSI BADO INAKULILIA


.
Na Berensi Alikadi.
30/8/2013
LEO ni mwaka mmoja tangia kifo cha aliyekuwa mwandishi wa kituo cha chanel ten mkoani Iringa Marehemu Daudi Mwangosi.
Kama tunavyofahamu Mwangosi aliuwawa na polisi sept 2mwaka 2002 akiwa kazini huko katika kiijiji cha Nyaroro wilayani Mfindi mkoani Iringa ambako alikuwa amekwenda kuandika habari za mkutano wa chama cha demkorasia na maendeleo [Chadema].
Siku hiyo Mwangosi alikwenda pale kijijini akiwa katika majukumu yake ya kikazi ambako alitaka kuwahahabarisha wananchi kilichosemwa katika mkutano huo lakini maskini hakuweza kutimiza lengo lake na badala yake polisi kwa amri ya Kamuhanda walimugeuza uji.
Hakuna ubishi katika hilo kuwa mwandishi huyo hakuuwawa na polisi kwani taarifa za awali toka kwa waandishi wenyewe wa mkoa wa Iringa zinasema kuwa aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa huo Michael Kamuhanda ambaye bado serikali inamkumbatia aliitisha mkutano na waandishi wa habari ofisini kwakwe  na katika mkutano huo baada ya kueleza adhima yake ya kuuzuia mkutano wa chadema,marehemu mwangosi alionekana kuumuliza maswali mengi ambayo yalionekana kumukera kamanda huyo.
Maswali ya Mwangosi kwa kamanda  huyo wa polisi huenda ndiyo yaliongeza chuki nap engine kuongeza hasira ya siku nyingi ambayo alikuwa nayo dhidi yake na hivyo akamuweka kiporo.
Taarifa zinaonyesha kuwa mara baada ya mkutano huo baadhi ya askari polisi waliwazuia waandishi wasiende kwenye mkutano huo jambo ambalo kwa mwandishi ni kosa kwani yeye pia anatakiwa kutimiza majukumu yake kama polisi walivyokwenda kwenye mkutano huo.
Habari zilieleza kuwa baada ya waandishi wa habari kufika katika eneo la kijiji cha Nyaroro na kufanikiwa kukusanya habari  walielekea kwenye eneo la kusini mashariki kupitia barabara kuu  Dar-Tunduma mahali ambalo ndipo alipouwawa mwangosi
Katika eneo hilo polisi waliwapiga waandishi wa habari na viongozi wa chadema pasipo sababu waandishi waliopigwa ni pamoja wale waliokuwa wakiandikia magazeti ya nipashe,mtanzania,Tanzania daima lakini adhima yao kuu ilikuwa kumua Mwngosi jambo ambalo walilitimiza pasipo kuacha shaka.
Siku hiyo ya tukio wakati baadhi ya waandishi walipokuwa wakipigwa na polisi, Mwangosi alimukimbilia kamanda Kamuahanda na kumuomba awamuru polisi  wake waache kumpiga mwandishi wa gazeti la nipashe Godfrey Mushi lakini hakumuelewa wala kumusikiliza  na badala yake walimushika na kumugeuzia kibao na kuanza kumpiga hadi askari mwingine alipomupiga na bomu tumboni lililosambaza mwili wake huku kamanda Kamuahanda akishuhudia na huo ndio ukawa mwisho wa maisha  ya Daudi Mwangosi.
Leo tunapotimiza mwaka mmoja tangia kifo cha mwandishi huyo hatuna budi kutafakali vitendo vya kikatili vinavyofanyiwa waandishi wa habari huku serikali ikiangalia pasipo kuchukua hatua.
Hivi ndugu msomaji hata wewe una kila sababu ya kujiuliza kulikuwa na sababu gani ya kuwazuia waandishi wa habari kwenda kwenye huo mkutano ,walikuwa na kosa gani hata kama wangepiga picha.
Katika hali ya haraka Napata picha kuwa siku hiyo polisi walikuwa na ajenda yao ya siri kama kawaida yao na ndio maana hawakutaka waandishi wafike huko na pingine huenda walipanga kabisa kuwauwa viongozi wa chadema na kuwepo kwa waandishi kulizima adhima hiyo na ndio maana hasira zao walimalizia kwa kuwapiga na kumuua Mwangosi.
Waandishi wa habari siku zote wako kazini kwa kufuata taratibu zao na namna walivyofundishwa kufanya kazi na wala hawafanyi kazi zao kwa kuamuliliwa na polisi lakini cha kushangaza sasa polisi wamekuwa wakiwakiwaingilia na hata kuwazuia kufanya kazi jambo ni ukiukwaji wa katiba ya nchi ibara ya 18.
Kwa miongo mingi sasa wananchi wamekuwa wakishuhudia namna waandishi wanavyonyanyaswa na jeshi la polisi,wako waliowahi kupigwa,kungo’lewa kucha,kumwagiwa tindikali kuporwa vifaa vyao vya kazi kama kamera na sasa mwaka jana dunia imeshuhudia waziwazi jeshi hili chini ya kiongozi aliyekabidhiwa kuuongoza mkoa akisimamia mwandishi anauwawa kwakweli inatisha na inaumiza sana.
Ni waandishi hawa hawa ambao kila siku polisi wanapokamata majambazi wale wasiowapa rushwa na vitu vile ambavyo huwa hawana mgawo huwaita na kuuza sura zao ili jamii iwaone kama kweli wanafanya kazi kumbe wengi wao ni mafisadi wakubwa.
Kilichonishangaza zaidi ni pale serikali hadi leo imemukingia kifua Kamuahanda huku kesi hiyo akipewa askari mdogo ambaye pia kila kukicha polisi wenzake wamekuwa wakimfanyia maagizo hata wakati wa kumpeleka mahakamani jambo linaloonyesha dhahili kuwa mauaji ya Daudi Mwangosi yalipangwa na wala si vinginevyo.
Nilitegemea sana rafiki yangu Nchimbi atamuchukulia hatua ya kinidhamu Kamuahanda lakini matokeo yake akahamishiwa makao makuu ya polisi ili kumficha huko wananchi wasifahamu kinachoendelea zaidi na hadi leo imekuwa kimya hakuna hata kiongozi wa polisi wala serikali wanaoweza kuzungumzia suala hili licha ya tasinia hii pia kuwa na wizara kamili.
Jeshi la polisi liliundwa kwa ajili  ya kulinda raia na mali zao wakiwemo waandishi wa habari lakini cha kushangaza leo jeshi hili limekuwa kinala wa kuuwa na wa kwanza pia kukimbilia kukanusha kwa kutumia vyombo vyao vya serikali kama vile TBC na magazeti ya uhuru na mzalendo ili kuwapoteza wananchi pasipo kufahamu kuwa wananchi leo hawadanganyiki.
Wakati leo wanahabari hapa nchini wanaungana na watanzania wengine katika kukumbuka mauji haya ya kinyama aliyofanyiwa Mwangosi hatuna budi kulaani kwa nguvu zetu na kulitaka jeshi la polisi liache kutumika kiasiasa.
Hatuna budi kuitaka serikali itamuke ni lini itawalinda waandishi wa habari wawapo kazini na ni lini polisi wataacha uhasama na waandishi wa habari maana kila kukicha chuki kati ya waandishi na jeshi hili inazidi kuongezeka kutoka na vitendo vya uonevu wanavyofanyiwa wakiwa kazini.
Polisi watambue kuwa waandishi ni sehemu ya jamii ya kitanzania nayo ina haki sawa katika nchi hii na pia inafahamu maovu mengi na kama siku ikiamua kumwaga mboga basi hapo ndipo kutakapokuwapo kilio na kusaga meno.
Waache vitisho na kuingailia uhuru wa habari waache waandishi wafanye kazi zao kama tasnia uhuru wakumbuke hayo mabomu waliyotumia kumuua Mwangosi ni kodi yetu wananchi wakiwemo waandishi wa habari.
Leo familia ya Daudi Mwangosi inataabika lakini Kamuhanda anaishi maisha mazuri tena ameongezewa cheo kumbe polisi akiuwa mwandishi anaongezewa cheo na gari zuri la kiyoyozi hakuna hatua zilizochukuliwa na lakini naamini mungu yupo na damu ya Mwangosi itaendelea kumulilia siku hadi siku.
Waandishi wa habari leo hawana uhuru wa kufanya kazi katika nchi yao,hawana uhuru wa kuhudhulia hata mikutano ya kisiasa hususa ni ile ya vyama vya upinzani kasoro ya chama cha mapinduzi ambacho hata kama kikikosea polisi husema amina’’.
Ndiyo maana waandishi sasa tunaomba katiba ijayo waandishi watambuliwe na uwe mhimili kamili kama mihimili mingine kwani wana mchango mkubwa katika nchi hii na tunataka tuachwe huru na hatutaki kuingilia na polisi na kupigwa mabomu pasipo sababu.
Tunataka polisi waache kutugeuza kama kiti moto bali watautambue na watuheshimu kama wanavyoheshimu hao wanaowatuma kutupiga mabomu na wafahamu kuwa hiyo kazi ina mwisho na mwisho wao siku zote huwa ni mbaya na wengi wao wamekuwa wakikimbilia kuomba msaada kwa waandishi ili waweze kuandikiwa mambo yao pindi wakwamapo kulipwa mafao yao ya kusitaafu uhamisho nk.
Sisi wote ni watanzania wala polisi wasijione wao wako juu ya sheria na kutukandamiza lazima waandishi wote tuungane kwa nguvu zetu na tukatae biashara hii ya polisi kutufanya sambusa kila mtu ana haki ya kutimiza wajibu wake kikazi hivyo hata mwandishi kuhudhulia mkutano ni haki yake na tunataka polisi msituchagulie cha kuandika nyie milisomea mguu pande na sisi tulisomea kuandika hivyo tuacheni tulivyo na kalamu zetu na nyie na bunduki zenu lakini mkijua hiyo ni kodi ya walalahoi na siyo ya kwenu.
Tunayo kila sababu ya kulaani vitendo viovu dhidi ya polisi wanavyofanyiwa waandishi kumbukeni haya manyanyaso hayakuanzia kwa Mwangosi tu bali wako wengi akina Katabalo na wengine mnaowafahamu sasa lazima tusema manyanyaso ya polisi dhidi ya wanahabari sasa basi.
Damu ya Mwangosi iliyomwagika akiwa anatetea kazi yake iwe chachu kwa waandishi wote hapa nchini,tutafakali kwa pamoja juu ya maisha yetu ya kila siku na namna tunavyowindwa ili roho zetu ziondoke,lazima tumukumbuke mwenzetu kwa uchungu mkubwa na tuongeze msikamano katika kudai haki yetu ya kupata habari mahali popote.
Kamwe ushujaa wako hautasaulika katika tasinia ya habari kila kizazi naamini kitasoma historia yako ambayo itaandikwa kila kukicha na wapenda haki sisi tunaamini ulikufa katika haki na tutaendelea kukumbuka kila siku na mchango wako katika habari utakumbukwa daima siku zote.
Lakini kwa jeshi la polisi hususa ni kamanda Kamuhanda lazima atatmbue kuwa kila kukicha damu ya Mwangosi itaendelea kumulilia kila siku maana bila yeye Mwangosi bado tungekuwa naye.
Tunasema Mwangosi amepumzika lakini tuliobaki tutaendeleza mambano ya kutetea uhuru wa kupata habari pasipo kuogopa vitisho vya polisi.
Pumzika kwa amani Kamanda Mwangosi.


No comments:

Post a Comment

Comments System

disqus

Disqus Shortname

msora

Popular Posts

Header Ads

ad