NA Berensi
Alikadi,Bunda.
1/9/2013
WANANCHI vijiji vya kata ya Butimba katika tarafa ya
Kenkyombyo wilayani Bunda mkoani Mara wanaishi kwa hofu kubwa kutokana na
kuibuka kwa vitendo vya kishirikina katika vijiji hivyo.
Wakiongea na
Tanzania daima ilipotembelea vijiji hivyo jana wananchi hao wamedai kuwa kwa
muda wa wiki nzima sasa kumekuwepo na vitendo vya kishirikiana ambapo watu
wasiofahamika wamekuwa wakienda katika vijiji hivyo majira ya usiku na
kuwanajisi wanawake na bila wao kujitambua.
Aidha
walifafanua kuwa baada ya watu hao kuwafanyia vitendo hivyo huchukuwa pesa na
kuondoka ambapo wao huwa hawajitambui kabisa.
Baadhi ya
wananchi wa kijiji cha Buramba wameliambia Tanzania daima kuwa tatizo hilo siyo
kwa akina mama tu bali watu hao ambao kwa lugha ya kijita wanafahamika kama
[wafafuti] wamekuwa wakiwalawiti hata wanaume jambo ambalo limezuia hofu kubwa.
‘’Kwakweli
Mwandishi hali hii inasikitisha sana watu hawa haifahamiki wanakuja saa ngapi
isipokuwa tu asubuhi wewe unakuta umenajisiwa na una mbegu za kiume sasa
inashangaza hapo awali walianzia kwa wanawake lakini sasa hata wanaume’’alisema
mtu huyo ambaye hakutaka atajwe gazetini.
Diwani wa
kata hiyo Ngunya Msalaba amekiri kuwepo
kwa hali hiyo na kwamba mnamo agost 26 mwaka huu majira ya saa tano usiku kaya
tano za wafanyakazi wa kiwanda cha kuchambua pamba cha Bulamba walikumbana na
dhahama hiyo
Msalaba
alisema kuwa baada ya kuwepo kwa matukio hayo waliamua kufanya mkutano wa
hadhara katika kijiji hicho ambapo walikubaliana mambo mbalimbali ikiwa ni
pamoja na kuwarudisha makwao waganga wote wa kienyeji ambao wamehamia katika
vijiji vya kata hiyo.
Alisema kuwa
jambo lingine walilokubaliana na pamoja na wageni wote wanaokwenda kufanya kazi
katika kiwanda hicho wawe na vitambulisho vinavyotambulika na wavipeleke kwa
viongozi wa kijiji hicho.
Sambamba na
hilo diwani huyo alidai kuwa wameanzisha jeshi la sungusungu kwa ajili ya kulinda usiku na mchana ili kama
watamuona mtu mgeni waweze kumuhoji.
‘’Lakini pia
tumeunda jeshi la sungusungu ambalo litalinda mchana na usiku ingawaje pia ni
kazi ya ziada maana watu wenyewe wanakuja usiku kazi ipo mimi sijawahi kusikia
jambo hili’’alisema diwani huyo.
Kufutia hali
hiyo diwani huyo ametoa wito kwa wananchi hao kuwa na subira wakati wakiendelea
kulifanyia uchunguzi suala hilo ambalo alisema linatia shaka maisha ya wananchi
wa kata hiyo.
Tatizo hilo
la wananchi kuingilia na kunajisiwa kishirikina limeshamili sana katika kipindi
cha miaka zaidi ya miwili hasa katika jimbo la Mwibara ambako hivi karibuni
wananchi wa vijiji vya Kasahunga walikumbwa na tatizo hilo
Mwisho
No comments:
Post a Comment