NA Berensi
Alikadi-Serengeti.
16.9.2013
SERIKALI
imesisitiza adhima yake ya kuendelea kulilinda bonde la mto Mara kutokana na
umuhimu wa bonde hilo kwa nchi za Kenya na Tanzania kiuchumi.
Kauri hiyo
ya serikali imetolewa na waziri mkuu Mizengo Pinda wakati alipokuwa akihutubia
wananchi wa Kenya na Tanzania kwenye
kilele cha maadhimisho ya Mara day zilizofanyika katika uwanja wa kumbukumbu ya
Sokoine mjini Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara.
Waziri mkuu
alisema kuwa viongozi wanatakiwa
kuendelea kuelimisha umma juu ya suala zima la uhifadhi wa mazingira katika mto
mara kwani ndiyo njia pekee ya kununusuru bonde hilo.
Alisema kuwa
Tanzania inashirikiana na Kenya kwa sababu chemichemi za mto Mara zimeanzia
kwenye milima ya Mau nchini Kenya na kupitia katika hifadhi za masai Mara hadi
Serengeti kwa upande wa Tanzania.
‘’Tanzania
kwa kutambua ukubwa wa jambo hili tumekubali kutii protoko ya kulinda mto Mara
na tutauheshimu’’alisema Pinda.
Alifafanua
kuwa katika sera ya maji ya mwaka 2002 na sheria usimamizi wa maji ya mwak 2009
vimetambua bonde hilo kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo hivyo tutumie
maji vizuri na tunawahakikishia wenzetu wa Kenya kuwa tutaendelea kuheshimu
makubaliano hayo.
Aliongeza
kuwa pamoja na bonde hilo kuwepo lakini bado zipo changamoto mbalimbali
zinazolikabili ikiwa ni pamoja na uharibifu wa mazingira,kilimo kando kando ya
bonde hilo na uchomaji moto ovyo ambavyo aliwagiza viongozi wa maeneo hayo
kuhakikisha wanasimamia visitokee tena.
Kwa upande
wake naibu waziri wa maji,Mhandisi Binilith Mahenge alisema kuwa lengo kuu la
kuanzishwa kwa kamisheni ya bonde la mto Mara ni kuhamasisha jamii katika
kuhifadhi mistu na vyanzo vya maji na kwamba hadi sasa jumla ya miradi 122 ya
uhifadhi wa mazingira imeanza kutekelezwa.
Awali
akimkaribisha waziri mkuu kuongea na wananchi,mkuu wa mkoa wa Mara John Tupa
alisema kuwa pamoja na mambo mengine sherehe hizi pia zinahusha tukio kubwa la
wanyama aina ya nyumbu ambao uhama makundi kwa makundi toka hifadhi ya masai
Mara na kuja katika hifadhi ya Serengeti.
Mwisho
No comments:
Post a Comment