NA Berensi
Alikadi-Bunda.
6.10.2013
SERIKALI
wilayani Bunda imeseme itaendelea kusaidiana na madhehebu ya dini wilayani humo
ili kuiweka wilaya hiyo katika hali ya
amani na utulivu.
Kauri hiyo
ya serikali imetolewa juzi wakati wa
misa ya kumuwekea mikono mchungaji mpya wa kanisa la Menonite la mjini
Bunda,Stafa Nashon Waryuba.
Mkuu wa
wilaya hiyo,Joshua Mirumbe ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasim katika sherehe
hizo alisema kuwa madhehebu ya dini katika wilaya hiyo yanafanya kazi kubwa ya
kuwaweka wananchi katika imani hivyo hayana budi kuheshimiwa.
Alisema kuwa
kanisa la Menonite lina histolia kubwa hapa nchini na kwamba serikali inatambua
mchango wake katika kuwaandaa wananchi waweze kumutumikia mungu kwani amani
iliyopo hapa nchini imetokana na madhehebu ya dini
‘’Nafurahi
sana kuwa leo Nashon sasa amekuwa mchungaji na kuanzia sasa tutakuita mchungaji
lakini ufahamu kuwa kazi ya uchungaji ni ngumu maana unadili na waumini kila
wakati hivyo ni lazima ujitume na sisi serikali tutakupa msaada kamatunavyoyapa
madhehebu mengine.’’alisema Mirumbe.
Awali askofu
wa kanisa la menonite jimbo la Serengeti,Christopher Ndege alisema kuwa kanisa
linataka viongozi imara na shupavu wanaoweza kulisimamia na akamtaka mchungaji
huyo awe mfano bora kwa waumini wa kanisa hilo.
Naye
mchungaji Nashon akiwashukuru waamini wa kanisa hilo na makanisa mengine
yaliyohudhulia hafla hiyo alisema kuwa atatumia karama yake aliyopewa na
mwenyezi mungu katika kulitumikia kanisa hilo na jamii ya Kitanzania na
akawaomba waendelee kumuombea na kumpa ushirikiano.
Kabla ya
kuwekewa mikono na askofu ndege,mchungaji Nashon alikiri mbele ya waaumini wa
kanisa hilo na kula kiapo cha uaminifu kama mchungaji na kisha alipewa hati
maalumu ya uchungaji na askofu huyo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment