NA Berensi Alikadi-Bunda
23/10/2013
WACHIMBAJI
wawili wa madini katika mgodi ulioko katika kijiji cha Kamukenga wilayani Bunda
mkoani Mara wamefariki dunia baada ya kufukiwa na kifusi.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo diwani wa kata ya Kiwasi mahali kilipo kijiji hicho,Lawi
Nyamajeje alisema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa kumi na mbili
alifajili.
Alisema kuwa
siku hiyo ya tukio wachimbaji hao waliingia katika shimo hilo kwa ajili ya
kuchimba dhahabu na kwamba wakiwa wanaendelea na kazi hiyo ghafula
walipolomokewa na kifusi.
Diwani huyo
alifafanua kuwa baada ya kufukiwa na kifusi hicho jitihada za kuwaokoa
zilishindikana na kwamba walipofanikiwa kuwatoa tayari walikuwa wameshakufa.
Aliwataja
waliokufa kuwa ni,Paskali Wiliam 16 mkazi wa kijiji cha Kamukenga na Robert
Kamoga 18 mkazi wa wilayani Serengeti mkoani Mara.
Aidha
aliongeza kuwa katika tukio hilo watu wawili walijeruhiwa vibaya na kwamba
walikimbizwa katika hosptali ya wilaya ya Bunda kwa ajili ya matibabu.
Hata hivyo
diwani huyo alisema kuwa baada ya tukio hilo waliweza kukaa na mkuu wa
upelelezi wa makosa ya jinai wilaya ya Bunda pamoja na wachimbaji ili kuona
namna ya usalama wa migodi hiyo ya wachimbaji wadogo wadogo kuendeshwa kwa
usalama zaidi.
Polisi
wilayani hapa wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba hakuna mtu yeyote
anayeshikiliwa kutokana na tukio hilo
Mwisho
No comments:
Post a Comment