Na Berensi
Alikadi,Tarime
27.10.2013.
MIFUGO 184
kutoka kaya 22 za Kijiji cha Kegonga kata ya Nyanungu wilayani Tarime mkoani
Mara imepigwa risasi na kuawawa na askari wanaosadikiwa kutoka kikosi cha
kupambana na ujangili katika hifadhi ya taifa ya Serengeti.
Tukio hilo
lilitokea juzi saa 7 mchana ambapo
mifugo iliyopigwa risasi ni ng’ombe 67,
mbuzi 113 na kondoo wanne waliokuwa wakichunga katika bonde la Nyanungu karibu
na hifadhi hiyo na kwamba miili mingine ya mifugo hiyo tayari imeliwa na fisi.
Imeelezwa
kuwa kabla ya kufanya unyama huo askari hao waliwakamata watu watatu, Maria
Chacha, Matinyi kemore na Bhoke Tarage waliokuwa wakichunga mifugo hiyo na kutokomea nao ndani ya hifadhi
huku wakitelekeza mifugo hiyo ikiwa imekufa.
Akiongea na gazeti
jana na kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji
cha Kegonga Chacha Tugara alieleza kuwa
askari hao walikuwa wamevaa sare za askari wa hifadhi ya wanyama pori.
alidai kuwa
askari hao ambao idadi yao haikufahamika mara moja walianza kuswaga mifugo hiyo
kuwatoa walipokuwa wakichunga katika mwinuko mmoja na kuzielekeza katika bonde
hilo kabla ya kuzifyatulia risasi.
Hata hivyo
mwenyekiti huyo alikanusha mifugo hiyo kuingia ndani ya hifadhi na kwamba
mifugo hiyo ililazimishwa huku akifafanua kuwa hata kama ingekuwa imeingia ndani
ya hifadhi lakini si haki kuipiga risasi na kwamba mifugo ilipokuwa ikiingia
ndani ya hifadhi kwa bahati mbaya wahusika walikuwa wakitozwa faini na walikuwa wakilipa faini hizo na kuchukua
mifugo yao.
“Kwakweli
nisema tu kwamba serikali itambue kuwa
hii nchi ni yetu sote hivyo kuwatendea wananchi vitendo hivi vya kinyama si
haki na huu ni uvunjaji wa haki za binadamu na wanyama” alisema Mwenyekiti Huyo.
Alisema
pamoja na mifugo hiyo kupigwa risasi hadi jana hakuna vyombo vya usalama
vilivyofika katika eneo hilo kwa uchunguzi licha ya taarifa hizo kupelekwa
polisi
Alitaja
majina ya idadi kaya na ng’ombe zao zilizopigwa risasi kwenye mabano kuwa ni Magaiwa
Kemore(7), Ryoba Nyamohanga(2), Mwita Ryoba(3), Daniel Giboswa(2), Chacha
Marwa(5), Nchaguru Mokami(3), Buraga Buraga(1).
Wengine ni
Mtatiro Marwa(3),Mwita Nyamohanga(3), Charles Petro(4), Chacha Keroka(3),
Matiko Wantahe(5), Chacha Matiko(2), Sasi Marwa(1), Mwita Gugura(6), Getaro
Teroge(4), Chacha Paulo(3).
Alitaja
wengine ni pamoja na Marwa Mwera(2), Juma Kemore(3), Makuru Chacha(2), wambura
Nyamhanga(1) na Waisiko Mwita(2) na kwamba wote ni wakazi wa Kijiji cha
Kegonga.
Tanzania
daima jana imemtafuta mkurugenzi wa Tanapa,Allan Kijazi ii aweze kuzungumzia
tukio hilo lakini ambapo alisema yuko nchini China kikazi na kutaka suala hio
ailizwe mkuu wa hifadhi ya Serengeti
Mkuu wa
hifadhi ya Serengeti aliyejitambulisha kwa jina la Mwakilema alipoulizwa kuhusu
tukio hilo alisema kuwa yeye hana taarifa na kwamba taarifa za doria
inayoendeshwa hivi sasa yupo msemaji wake ambaye ni meja wa jeshi ambaye
hakutaka kumtaja.
Tukio hili
linatokea miezi michache baada ya tukio lingine linataka kufanana na hilo
kutokea katika Kijiji cha Mariwanda wilayani Bunda ambapo askari kutoka hifadhi
ya Serengeti kuswaga mifugo zaidi 50 ndani ya mto Rubana na kufia majini.
…………………………….mwisho………………………………………..
No comments:
Post a Comment