Wednesday, April 2, 2014

WADAU WA AFYA SIMIYU WARIDHIA KUTUMIKA MFUMO WA TIBA KWA KADI.



WADAU WA AFYA SIMIYU WARIDHIA KUTUMIKA MFUMO WA TIBA KWA KADI.

Na Berensi Alikadi. Simiyu,

Wadau wa afya katika halmshauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu,  wameridhia kutumika kwa mfumo mpya wa utoaji wa huduma za afya kwa njia ya tiba kwa kadi (TIKA), mfumo unaolenga kupunguza kero ya upatikanaji wa dawa pamoja na vifaa tiba katika vituo vya afya na hospitali.

Wadau hao wamefikia uamuzi huo kwenye washa iliyofanyika kwenye ukumbi wa kanisa katoliki mjini Bariadi.

Mbali na kuridhia kutumika kwa mfumo huo mpya, ambao uko chini ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ( NHIF), wadau hao wamedai  kuwa ili kupatikana mafanikio ya kutumika kwa mfumo huo ni vema  kuwepo kwa usimamizi mkubwa wa fedha za zitakazotokana na huduma hiyo.

Wakiongea kwa nyakati tofauti walisema uanzishwaji wa mfuko wa afya ya jamii Mjini (TIKA),  kutasaidia wananchi kuweza kutibiwa kwa uarahisi kuliko ilivyo sasa ambapo wananchi hao uangaika katika kutafuta fedha za matibabu.

Walifafanua  kuwa mfumo huo wa tiba kwa kadi malengo yake yana faida kubwa kwa wananchi ambao hawana uwezo wa kuweza kumudu gharama za matibabu, ambapo walieleza kuwa usimamizi wa fedha za wanachama wa huduma hiyo ni lazima kuwa mkubwa.

“ tunipongeza serikali kwa kuleta mfuno huu, sisi hatuna shaka ikiwa utaletwa kwa wananchi wetu, kwani unalenga kutatua kero waliyonayo ya kila siku katika kupata huduma za afya, pamoja na hayo ni lazima usimamizi wa fedha za wananchi wetu watakao kuwa wananchama katika mfumo huu, unatakiwa kuwa mkubwa sana ili fedha zao zisitafunwe na wachache” Alisema Selina Deusi.

 Akitoa maelezo ya juu ya faida ya mfumo huo Mwakilishi wa Mkurugenzi mkuu wa Bima ya Taifa ya Afya Elltruder Mbogolo, alisema kuwa lengo la kuletwa kwa mfumo huu, itasaidia kupungua kwa kero za upatikanaji wa dawa pamoja na vifaa tiba katika vituo vya afya na ospitali.

Semina hiyo iliyokuwa imeudhuliwa na wadau mablimabli wakiwemo, viongozi wa dini, wazee maarufu, viongozi wa vyama vya siasa, vijana, madiwani wa halmshauri ya mji, wanawake, pamoja na waremavu, ambapo mfumo wa Tiba kwa Kadi (TIKA) umelenga kutumika katika halmshauri za miji, manispaa pamoja na jiji.

Akifungua washa hiyo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Simiyu,Katibu Tawala wa mkoa huo,Mwanvua Jirumbi amewataka viongozi wa halimashauri zote za mkoa huo kuhakikisha wanasiamia ipasavyo mradi huo ili mradi huo uweze kuwanufaisha wananchi.

Washa hiyo ya siku moja iliwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi madhehebu ya dini,makundi ya walemavu na vyama vya siasa.

MWISHO

No comments:

Post a Comment

Comments System

disqus

Disqus Shortname

msora

Popular Posts

Header Ads

ad