Sunday, May 18, 2014

SERIKALI KUTOIPA KAZI YA KUCHIMBA MABWAWA,KAMPUNI YA NYAKILANG’ANI

NA MWANDISHI WETU MEATU SIMIYU,MEI 18,2014.


serikali imesema kuanzia sasa haitaipa kampuni ya ujenzi Nyakirang’ani
 ya mkoani mara kazi yeyote ya kuchimba mabwawa baada ya kampuni
kushindwa kukamilisha kazi za mabwawa mbalimbali hapa nchini.


kauli  hiyo ya serikali imetolewa wilayani meatu mkoani simiyu  na naibu
waziri wa maji,amosi makala mara baada ya kutembelea bwawa la mwanjoro
ambalo lilikuwa likijengwa na kampuni hiyo.

amesema  mkandarasi huyo ameonyesha kiwango cha chini katika ujenzi wa
mabwawa anayopewa na kwamba kuanzia sasa hatapewa kazi yeyote ya
ujenzi wa mabwawa na wizara hicho hapa nchini kwani  amekuwa
mkandarasi mbabaishaji na asiye na uwezo licha ya kupewa kazi hizo na
wizara.
‘’Nimefika mwenyewe nimejionea hali halisi ilivyo na nimeacha watalaam
wa wizara yangu waweze kufanya tathimini na watuleteea kabla
hatujasoma bajeti na mkandarasi huyu nimesema yeye na wizara yetu sasa
basi hatuwezi kupata hasara kwa kuwavumilia wakandarasi
wababaishaji.’’alisema Makala



mkuu wa wilaya hiyo.Rose mary kirigini
alimueleza naibu waziri huyo bwawa hilo lilianza kujengwa tangia mwaka
2009 hadi sasa na kwamba taarifa imekuwa ikionyesha kuwa limekamilika
kwa asilimia 80 jambo ambalo si kweli.na kwamba wakati umefika sasa
,kwa wananchi wa vijiji hivyo kulitumia bwawa hilo kwani wametaabika
kwa muda mrefu sana


Awali mhandisi wa maji toka sekretalieti ya mkoa,Gibson Kisaka amesema
 hali ya upatikanaji wa maji katika mkoa huo haitoshi kutokana na
vyanzo vingi kuwa na maji yenye madini ya frolide na kwamba
wanaangalia uwezo wa kuongeza idadi ya mabwawa ili yaweze kukidhi
haja.

kwa upande wao wananchi wa vijiji vya mwanjoro  na jinamo mahali
lilipo bwawa hilo wameiomba serikali kulisimamia bwawa hilo ili liweze
kukamilika kwani wamekuwa wakipata shida ya maji.
 Wananchi hao wamesema kuwa wamekuwa wakifuta maji kwa umbalimrefu kwa
kutumia wanyama  aina ya punda na kwamba bei ya maji kijijini hapo ni
shilingi mia tano kwa ndoo moja.
Makala anatembelea maeneo mbalimbali yaliyo na kero ya maji kabla ya
kuwasilishwa kwa bajeti ya wizara hiyo  tarehe 30mwezi huu.
mwisho
Why this ad?Ads –
Uroa Bay Beach Resort Is what we do best

No comments:

Post a Comment

Comments System

disqus

Disqus Shortname

msora

Popular Posts

Header Ads

ad