Kiasi watu 13, ikiwa ni pamoja na mshambuliaji wa kujitoa muhanga , wamekufa leo katika mashambulizi mawili tofauti katikati ya mji mkuu wa Iraq Baghdad.
polisi imesema shambulio la kwanza lilitokea katika wilaya ya kibiashara ya Bab al-Sharj ambako bomu liliripuka katika gari iliyoegeshwa. Watu wanane waliuwawa na wengine 40 wamejeruhiwa.
Mshambuliaji wa kujitoa muhanga , akivalia mkanda wa miripuko , alijiripua katika eneo la Wathba , akijiuwa binafsi na watu wengine wanne. Maafisa wa polisi ni miongoni mwa waliouwawa.
Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo hadi sasa. Mashambulizi ya hapo kabla yamedaiwa kutekelezwa na kundi la Dola la Kiislamu, ambalo linadhibiti maeneo makubwa kaskazini na magharibi ya Iraq.
CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment