Kikosi cha ulinzi wa rais nchini Burkina Faso kimetangaza mapinduzi leo siku moja baada ya kuwakamata rais wa mpito na waziri mkuu jana, wakati nchi hiyo ikijitayarisha kwa uchaguzi mkuu wa kwanza tangu kupinduliwa kwa kiongozi wa nchi hiyo Blaise Compaore.
Akitangaza mapinduzi luteni kanali Mamadou Bamba amesema mazungumzo yanafanyika hivi sasa kuunda serikali itakayoiongoza nchi hiyo katika uchaguzi wa amani.
Kumekuwa na maandamano mitaani nje ya Ikulu ya rais na Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa limeshutumu vikali kukamatwa kwa viongozi hao na kutaka waachiliwe haraka.
Wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa rais wenye mafungamano na rais wa zamani Blaise Compaore waliingia katika mkutano wa baraza la mawaziri jana na kumkamata rais Michel Kafando, waziri mkuu Isaac Zida na mawaziri wengine wawili.
Kaimu spika wa bunge la Burkina Faso Cherif Sy ameshutumu vikali leo kile alichosema kuwa ni mapinduzi nchini Burkina Faso.
CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment