Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
SERIKALI
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia
itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika.
Mkutano
huo utakaofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete utafanyika tarehe 4 – 5 Septemba, 2015 katika
Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Kauli Mbiu ni “Tumia Takwimu Huria Kuendeleza Afrika” (Developing
Africa Through Open Data).
Washiriki
takribani 400 kutoka Serikalini, Asasi za Kiraia, Sekta Binafsi,
Taasisi za Elimu ya Juu na Washirika wa Maendeleo kutoka ndani na nje ya
Nchi wanatarajiwa kushiriki.
Miongoni
mwa washiriki kutoka Serikalini ni pamoja na Wakurugenzi kutoka Idara
za Sera na Mipango, Wakuu wa Vitengo vya TEHAMA na Maofisa Takwimu
Waandamizi wa Wizara zote.
Mkutano
wa Takwimu Huria kwa Kanda ya Afrika ni wa kwanza wa aina yake Barani
Afrika Tanzania ikiwa nchi ya kwanza kuwa mwenyeji.
Heshima
hiyo imetokana na Tanzania kujiunga na Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli
za Serikali kwa Uwazi (Open Government Partnership – OGP) unaolenga
kuifanya Serikali kuwa wazi zaidi na hivyo kuleta uadilifu na
uwajibikaji katika kuwahudumia Wananchi.
Katika
utekelezaji wa Mpango wa OGP, Tanzania iliweka kipaumbele katika
kuanzisha Tovuti ya Takwimu Huria itakayoweka wazi takwimu mbalimbali za
Serikali na Taasisi zake.
Madhumuni ya Mkutano ni kujadiliana kuhusu mfumo wa Takwimu Huria na jinsi utakavyoleta maendeleo hususan kwa nchi za Afrika.
Mkutano
utawawezesha wadau kujadiliana na kubadilishana uzoefu kuhusu mfumo wa
Takwimu Huria na kuona jinsi gani Sera za nchi zenye mfumo huo
zinavyofanya kazi na kusimamia viwango vya upatikanaji wa Takwimu Huria.
Aidha,
Mkutano huo utaihusisha sekta binafsi na wadau wengine katika matumizi
ya Takwimu Huria katika kuleta maendeleo ya kasi zaidi Barani Afrika.
Washiriki
watajadili jinsi ya kukuza na kuimarisha matumizi ya Mfumo wa Takwimu
Huria katika kutoa huduma kwa wananchi hasa katika sekta ya Huduma za
Jamii za elimu, afya, maji na kilimo.
Tunaomba ushirikiano wenu.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA MASHAURIANO YA WAWAKILISHI WA KAMATI YA KUDUMU YA UMOJA WA AFRIKA (AU) NA WATAALAMU WA HAKI NA SHERIA, JIJINI ARUSHA.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Kamati ya Kudumu ya Umoja wa
Afrika( AU) wakati alipokuwa akiwasili kwenye Hoteli ya Mount Meru
Jijini Arusha kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Mashauriano kati ya
Wawakilishi wa Kamati ya Kudumu ya Umoja wa Afrika( AU) na Wataalamu
wa Masuala ya Haki na Sheria, uliofanyika kwenye Hoteli hiyo uliokuwa
ukijadili kuhusu kuimarisha demokrasi, utawala wa sheria na masuala ya
uchaguzi. Wa tatu (kulia) ni Jaji Mkuu Mstaafu Agustino Ramadhan.
Picha na OMR


Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
(kulia) akiteta jambo na Rais wa Mahakama ya Afrika, Jaji Mkuu Mstaafu,
Agustino Ramadhan, wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo wa Mashauriano kati
ya Wawakilishi wa Kamati ya Kudumu ya Umoja wa Afrika( AU) na
Wataalamu wa Masuala ya Haki na Sheria, uliofanyika kwenye Hoteli ya
Mount Meru jijini Arusha jana Sept 2, 2015 ambao ulikuwa ukijadili
kuhusu kuimarisha demokrasi, utawala wa sheria na masuala ya uchaguzi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
(kulia) akikabidhiwa zawadi na Rais wa Mahakama Afrika Jaji Mkuu
Mstaafu, Agustino Ramadhan, wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo wa
Mashauriano kati ya Wawakilishi wa Kamati ya Kudumu ya Umoja wa
Afrika( AU) na Wataalamu wa Masuala ya Haki na Sheria, uliofanyika
kwenye Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha jana Sept 2, 2015 ambao
ulikuwa ukijadili kuhusu kuimarisha demokrasi, utawala wa sheria na
masuala ya uchaguzi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
na Rais wa Mahakama ya Afrika, Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Agustino
Ramadhan, wakisalimiana na baadhi ya washiriki wa mkutano huo baada ya
kufunguliwa rasmi jana jijini Arusha.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
Rais wa Mahakama Afrika, Jaji Mkuu Mstaafu, Agustino Ramadhan, wakiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka
mataifa mbalimbali ya Afrika baada ya ufunguzi jana jijini Arusha. Picha
na OMR
No comments:
Post a Comment