
Maandamano nchini Burundi
Watu wawili wameuawa katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura kufuatia makabiliano makali ya risasi Jumanne Usiku.
Kumekuwa
na machufuko zaidi katika wilaya zilizoadhirika kwenye maandamano ya
kupinga uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza wa kuwania muhula wa tatu.
Baadhi ya mitaa mjini humo zimezingirwa na maafisa wa ulinzi.
Nchini
Tanzania, idadi ya wakimbizi kutoka Burundi, inaendelea kuongezeka kila
uchao. Umoja wa Mataifa umesema kuwa wakimbizi mia nne kutoka Burundi
huvuka mpaka na kuingia Tanzania kila siku.
Kufikia
sasa zaidi ya wakimbizi elfu tisini wamekimbilia nchi jirani ya Tanzania
tangu mzozo wa kisiasa kuanza nchini Burundi, Aprili mwaka huu.
Idadi ya watu mashuhuri wanaouawa nchini humo imekithiri katika siku za hivi karibu.BBC
No comments:
Post a Comment