RUNGWE CHAUUMA NDIO CHAMA CHA KWENDA IKULU
Published in
Siasa

CHAMA cha
Chaumma kimezindua kampeni zake kitaifa huku kikidai kuwa ndicho chama
pekee Chenye nguvu kuliko Vyama vya Ukawa chini ya mgombea wake Edward
Lowasa na chama cha mapinduzi ( CCM) chini ya Dr John Magufuli
Huku Mgombea Urais akiahidi Ujenzi wa kiwanda cha magari Dar es salaam
Katibu
mwenezi wa Taifa wa Chaumma na Mgombea jimbo la Ubungo Bw Kabendera
Mbehikya aliyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo
zilizofanyika viwanja vya Masenze jijini Dar es Salaam .
Alisema
kuwa watanzani wasilewe na mafuriko ya vyama vinavyojiita ni vyama
vikubwa alivyoviita vyama vinavyosindikiza Chama chao cha Chaumma Kwenda
Ikulu.
" Hivi
sasa kuna chama kimoja na nusu ndivyo vyenye nguvu katika uchaguzi huu
wa mwaka 2015 chama cha kwanza ni Chaumma na vyama vya CCM na Chadema na
washirika wake nusu kwa chama cha Chaumma... Hivyo kuwataka watanzania
kuchagua Chaumma na si vinginevyo"
Mgombea
mwenza wa chama cha Chaumma Issa Abas Husen alisema kuwa kukosekana kwa
viongozi bora ndiko kumelifikisha Taifa katika matatizo haya na kusema
dawa ya mafanikio ni kuchagua Hashim Rungwe kuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Alisema
kuwa Tanzania ni nchi tajiri ila imeshindwa kupiga hatua kutokana na
viongozi wabovu na utawala usio faa wa CCM na kuwa dawa sahihi ni
kuchagua chaumma pekee
Hata
hivyo alisema chama chake kimejikita zaidi katika sera za kuwakomboa
watanzania katika sekta kilimo na Viwanda,afya,elimu pamoja ,kukuza
ajira na umoja wa kitaifa
Kwani alisema ni aibu kwa Taifa kukosa kuwa na huduma bora za afya na kushindwa kuboresha sekta ya kilimo.
Huku
Mgombea Urais wa Chama hicho Mwanasheria Rungwe akiwaahidi watanzania
wanaoonewa kwenda kwake kupata huduma ya sheria ya bure.

Kampuni
ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, ambayo ni mdhamini mkuu wa Ligi Kuu
ya mpira wa miguu Tanzania bara leo imekabbidhi vifaa kwa timu
zinazoshiriki ligi hiyo yenye thamani ya shilingi milioni 490,00,000.
Akikabidhi
vifaa hivyo leo jijini Dar es salaam, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na
Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twisa alsiema kuwa kwa mara nyingine tena
katika kuhakikisha ligi ya soka nchini inaenda vizuri Vodacom inakidhi
vifaa mbalimbali vy a ligi ambavyo ni jezi za kawaida, jezi za mechi,
viatu na vifaa vingine vinayohitajika.
“Tunajisikia
furaha kukabidhi vifaa hivi siku ya leo tukiwaa tunatekeleza matakwa ya
mkataba wa udhamini, ni imani yetu kwamba timu zitakazoshiriki lii
zimejiandaa vya kutosha kwa msimu mpya 2015/2016” Alisema Twissa.
Twissa
alisema Vodacom inaendelea kudhamini ligi kuu kwa sababu soka ni mchezo
unaopendwa sana hapa nyumbani ukiwa na washabiki wengi hivyo inapenda
kuona wananchi ambao baadhi yao ni wateja wake wanapata buruddaniya
mchezo waupendao pia siku zote inaamini kuwa michezo ni ajira kubwa
duniani kote, ikiendelezwa inaweza kubadilisha maisha ya watu wengi na
taifa kunufaika kwa mapato makubwa ya kodi kutoka sekta hii.
Aliwataka
wadhamini wengine kujitokeza ili kuboresha zaidi ligi ya Tanzania na
kuongeza maslahi kwa wachezaji wanaoshiri katika ligi “Tukiunganisha
nguvu timu zetu zinaweza kuwa na wachezaji wa kimataifa pia ni muhimu
kwa wadau mbalimbali kuanza kuwekeza katika timu za vijana chipukizi kwa
kuwa vipaji vinaanza ngazi ya chini ambako vinapaswa kuibuliwa na
kuendelezwa” Alisema Twissa.

Mkurugenzi
wa Idara ya Mambo ya Nje, Balozi Salim Kombo amesema taarifa walizopata
nchini DRC zimesema Watanzania hao wanawakilisha taasisi ya Tabligh.
Bila ya kuwataja kwa majina, amesema hali zao ni salama na kwa sasa wanaishi chini ya uangalizi wa Serikali ya DRC.
Kombo
amesema waasi hao walitaka kulipwa Dola 40,000 ili kuwaachia Watanzania
hao, kiwango ambacho watekaji walipunguza baada ya kushindikana kupata.
Wakataka Dola 20,000.
Balozi Kombo amesema hatimaye wananchi hao waliachiwa bila ya kutolewa fedha yoyote baada ya kufanikiwa kwa ushirikiano wa serikali ya Tanzania na DRC.
Balozi Kombo amesema hatimaye wananchi hao waliachiwa bila ya kutolewa fedha yoyote baada ya kufanikiwa kwa ushirikiano wa serikali ya Tanzania na DRC.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula amesema taarifa
za kuachiwa kwa Watanzania hao zimepatikana usiku wa kuamkia leo kutoka
kwa Balozi wa Tanzania nchini Kongo, Antony Cheche.
Balozi
Mulamula amesema kutekwa kwa Watanzania hao, ni tukio lililotia hofu
viongozi kwa sababu ni mara ya kwanza kuwatokea Watanzania kokote kule.
Amesema
utaratibu wa kuwahamisha Watanzania kutoka Kivu na kupelekwa mjini Goma
unaendelea kufuatiliwa ili wapate kurejeshwa kwao baada ya kukabidhiwa
kwa Balozi Cheche aliyetarajiwa kuwasili mjini Goma leo.
Balozi
Mulamula amehimiza Watanzania wote wajenge utaratibu wa kufika ofisi za
kibalozi za Tanznaia wanaposafiri kwa shughuli mbalimbali ughaibuni.
Hiyo inaweza kusaidia kutoa msaada panapotokea dharura. Watanzania hao
waliotekwa DRC hawakuripoti rasmi serikalini kuhusu safari yao.

Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi na Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, James Mbatia
UMOJA wa
Katiba ya Wananchi (UKAWA) umesema hautajishughulisha na tuhuma zisizo
na kichwa wala miguu kwa kipindi hiki ambacho Watanzania wanataka
kusikia kauli za matumaini badala ya zinazopasua taifa.
Kauli
hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia wakati
akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya New Africa, kuhusu
tuhuma alizozitoa Dk. Willibrod Slaa ambaye amelaumu viongozi aliokuwa
nao Chadema kwa alichosema kimepokea viongozi waovu kutoka CCM.
Mbatia amesema mambo yanayofanywa na CCM kwa wananchi ni ya kutaka kuivuruga amani ya Watanzania, lakini dhamira yao inashindwa.
Lawama za
Dk. Slaa zililenga kumshambulia Edward Lowassa, ambaye ndiye
aliyejiunga Chadema akitokea CCM baada ya jina lake kukatwa kwenye
orodha ya waliojadiliwa kugombea urais.
Lowassa
ambaye ameteuliwa kuwa mgombea urais wa jamhuri ya Muungano kupitia
Chadema, akiwakilisha UKAWA, anaendelea kuzunguka nchi akifanya kampeni
ya kuomba ridhaa ya wananchi ya kuongoza taifa.
Mgombea mwenza wake ni Juma Duni Haji kutoka Zanzibar ambaye naye alikaribishwa Chadema akitokea Chama cha Wananchui (CUF). Dk. Slaa pia amemshambulia Frederick Sumaye, waziri mkuu mstaafu ambaye alihama CCM na kujiunga na kampeni ya Lowassa kuchukua uongozi wa dola.
Mgombea mwenza wake ni Juma Duni Haji kutoka Zanzibar ambaye naye alikaribishwa Chadema akitokea Chama cha Wananchui (CUF). Dk. Slaa pia amemshambulia Frederick Sumaye, waziri mkuu mstaafu ambaye alihama CCM na kujiunga na kampeni ya Lowassa kuchukua uongozi wa dola.

SERIKALI
imesaini mkataba wa makubaliano ya mkopo wa Dola za Marekani milioni
91.032 sawa na Sh bilioni 154.39 na Serikali ya Korea kwa ajili ya
ujenzi wa daraja jipya la Selander jijini Dar es Salaam.
Akisaini
mkataba huo, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum na Mkurugenzi Mtendaji
wa Benki ya Exim Korea, Yim Seong-hyeog alisema mradi huo ni muhimu kwa
uchumi wa Tanzania kwa kuwa eneo hilo lina foleni.
Salum
alisema mradi huo utaleta manufaa makubwa kiuchumi kwa kuwa utapunguza
msongamano ambao umekuwa ukiwachelewesha watu kwenye shughuli zao za
kila siku.
Alisema mradi wote mpaka utakapokwisha utatumia Dola za Marekani milioni 110.033 (Sh bilioni 186.6).
“Kwa
mradi mzima Korea imetoa asilimia 83 na Tanzania itatoa asilimia 17,”
alisema Waziri huyo na kusisitiza kuwa mradi huo utarahisisha kupunguza
msongamano.ningehangaa “Kwa mradi mzima Korea imetoa asilimia 83 na
Tanzania itatoa asilimia 17,” alisema Waziri huyo na kusisitiza kuwa
mradi huo utarahisisha kupunguza msongamano.

MGOMBEA
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli,
amewataka Watanzania kuwa makini wasije kudanganywa na matapeli wa
kisiasa watakaokuja na ahadi za uongo.
Akizungumza
katika Uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara jana, Dk Magufuli alisema
matapeli hao watakuja na ahadi nyingi, akawataka wananchi wawasikilize
na kuwapima kwa kauli na sifa zao kwa kuwa kuahidi ni rahisi kuliko
kutekeleza.
“Tusije
tukadanganywa na matapeli wa kisiasa, wakinamama mnafahamu matapeli wa
mjini walivyo na maneno matamu. Maendeleo ni changamoto na yataletwa na
sisi Wanamtwara,” alisema.
Miongoni
mwa matazamio ya Dk Magufuli ya Serikali atakayoiongoza kama
akichaguliwa kuwa rais, ni ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Mtwara
kupitia Songea mpaka Mbambabay, baada ya kuboresha Bandari ya Mtwara na
kuwa ya kisasa kama ya Dar es Salaam.
Alisema
bandari itaboreshwa ili pia iongeze ajira kwa wakazi wa mji huo huku
mizigo ya nchi za Zambia na Malawi, ikipitia mkoani humo.
Aidha,
alisema Serikali ya Awamu ya Tano atakayoiongoza, itajielekeza zaidi
katika kukuza uchumi kwa watu. Akizungumza katika mikutano mikubwa na
midogo katika wilaya za Newala, Tandahimba na Mtwara Vijijini kuhusu zao
la korosho, Dk Magufuli alisema katika uongozi wake, lazima korosho
ilete uchumi mzuri kwa wakazi wa Mtwara.
“Mimi
shahada yangu ya tatu (PHD) nimesomea korosho. Hakuna anayeweza
kunidanganya. Korosho siyo tu tunda la ndani, bali hata ganda ni uchumi
kwa kuwa linatengeneza gundi na dawa ya kuzuia kutu,” alisema Dk
Magufuli.
Alisema
korosho ya Tanzania ni tofauti na korosho nyingine duniani, kwa kuwa
yenyewe huanza kuvunwa wakati maeneo mengine duniani wamemaliza kuvuna.
Kwa
mujibu wa Dk Magufuli, katika uongozi wake hataruhusu korosho kuuzwa
ghafi nje ya nchi, bali Serikali itahakikisha kunajengwa viwanda
vitakavyotumia malighafi ya korosho ili zao hilo lipande bei.
Kuhusu
tatizo la stakabadhi ghalani ambalo limekuwa likilalamikiwa na wakulima,
Dk Magufuli alisema wamuachie yeye atahakikisha kero ya mfumo huo
inaondoshwa na wakulima hawadhulumiwi haki yao.

WATANZANIA
sita waliokuwa wameshikiliwa mateka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo (DRC), wameachiwa huru usiku wa kuamkia juzi.
Hayo
yalisemwa jana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula, wakati akizungumza na waandishi wa
habari Dar es Salaam.
Balozi
Mulamula alisema mateka hao walitekwa mwanzoni mwa mwezi uliopita
Mashariki mwa Congo, Kivu Kaskazini ambako walikwenda huko kwa masuala
ya dini ila kwa sasa wameachiwa huru.
“Hii ni
mara ya kwanza kwa tukio kama hili kutokea kwa Watanzania kutekwa ila
tunashukuru kwa sasa wapo huru na wanaelekea Goma kwa ajili ya kukutana
na Balozi wa Tanzania nchini Congo ili taratibu nyingine zifuatwe,”
alisema Balozi Mulamula.
Aliongeza
kuwa inasemekana walitekwa na kundi la waasi ambalo mpaka sasa
halijajulikana na walitoa masharti kuwa wanataka Dola za Marekani 20,000
(zaidi ya Sh milioni 60).
“Hakuna
fedha yoyote iliyotolewa ili kuwakomboa japo wapo watu waliojitokeza
kuchangia ikiwemo raia wa Congo na familia za mateka hao, lakini fedha
hizo hazijatolewa kwa waasi hao na hatujui imekuaje mpaka wakawaachia
huru,” aliongeza Katibu Mkuu.

MWENYEKITI
Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), James Mbatia, amewataka
Watanzania kumpuuza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa kwa kauli zake zilizojaa
uchochezi na propaganda za siasa.
Pia
alionya kauli za ovyo zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kwamba wapinzani wakishinda vyombo vya ulinzi vitachukua
nchi.
Alisema
jeshi la Tanzania linasimamia misingi yake na kiongozi yeyote
atakayeingia madarakani litafanya naye kazi kwa kuwa wote ni Watanzania.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kufafanua mambo mbalimbali
yalitamkwa na Dk. Slaa juzi, Mbatia alisema tuhuma alizozitoa kiongozi
huyo zinalenga kuleta mpasuko katika taifa na kuvunja amani ya nchi.
Alisema
hotuba nzima ya Dk. Slaa ililenga kumshambulia moja kwa moja Mgombea
urais wa Ukawa, Edward Lowassa kwa sababu amekuwa tishio kwake na kwa
CCM.
Mbatia
ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, alisema mara zote propaganda
kama hizo huwa zinafanywa na chama tawala ambacho kimekwisha kuona
viashiria vya kuondolewa madarakani kupitia sanduku la kura.
Mbatia
alitoa mfano kuwa kitendo cha Dk. Slaa kuwasingizia baadhi ya viongozi
wa dini kwamba walihongwa na Lowassa ili wamuunge mkono ni hatua ya
kuwataka waumini wasiwaamini viongozi wao jambo ambalo ni hatari kwa
amani ya nchi.
“Hoja
alizozitoa ni nyepesi ambazo Watanzania wanatakiwa kuzipuuza na
wasikubali mpasuko hasa unaoletwa kwa mlengo wa imani ya dini.

Trekta
karibu na mji wa Caen ikielekea katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris kwa
ajili ya kushiriki katika maandamano ya wakulima leo Alhamisi Septemba
3, 2015.
Na RFI
Wakulima
wa Ufaransa wana hasira na wamekua wakielezea ghadhabu yao. Wakulima hao
wanatazamiwa Alhamisi wiki hii kuandamana kwa wingi wakiwa na matrekta
yao hadi katika mji mkuu wa nchi hiyo, Paris.
Wakulima
kutoka wilaya 12 watashiriki katika maandamano hayo katika eneo la
taifa. Ujumbe wa wakulima hao utapokelewa leo mchan katika mji wa
Matignon, na mwingine utakwenda Bungeni ili kufikisha malalamiko yake
kwa wabunge. Maandamano haya yenye ushawishi mkubwa yametajwa kuwa ya
kihistoria na wafugaji wengi.
Wakulima
wanaelekea kwanza katika mji wa Paris ili waweze kutambuliwa. Wanahisi
kwamba hawaeleweki na wamekua wakipuuzwa, na raia watambuwe shida na
maisha duni yanayokumba wakulima.
" Kwenda
Paris ni pigo kubwa. Kuna matrekta 1500, kutakuwa na zaidi ya watu elfu 4
hadi elfu 5 mchana huu katika eneo la taifa. hali hii inaonyesha dhiki,
shida ya wakulima. Leo tunahitaji ufumbuzi wa kweli ambao ni endelevu
kwa ajili ya kutupa upya mitazamo na kutupongeza kwa kuamka asubuhi na
kufanya bidhaa bora za kilimo ", amesema Luc Smessaert, makamu wa rais
wa wa Shirikisho la Wakulima nchini Ufaransa (FNSEA).
Viwango
Mzozo huo
pia una sababu zaidi ya kiuchumi na kijamii. Bila shaka, wakulima hawa
hawategemei kitu cha ajaabu, lakini wanataka ufumbuzi katika madai yao.
Miongoni mwa madai yao, wanaiomba serikali punguzo la gharama ya kazi
wanaoifanya na gharama za wafanyakazi. Hizo ni moja ya pointi muhimu.
Ufaransa
inaendesha shughuli hii ya kiliomo kwa viwango wakati majirani zake,
Ujerumani na Hispania huzalisha kwa nafu na kuuza zaidi nje.
"
Serikali inapaswa kujitoa kwa kimuundo, na kutupunguzia mzigo wa gharama
na kutupunguzia pia viwango vya ilivyoweka. Na kusema kwamba nafasi kwa
Ufaransa ni kuwa na mifugo yenye maziwa, ng'ombe na nguruwe ",
amesisitiza Thierry Roquefeuil, rais wa Shirikisho la kitaifa la
Uzalishaji wa Maziwa.(P.T)
This
man has a secret about his health that you ill be shocked to learn.
Kazim Gurbuz is a Turkish yoga instructor that claims yoga and diet are
the key to a long life.

Afisa
wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Ezra
Ndangoya akimwelekeza sehemu ya kuweka sahihi Bw. Sironga Lowassa
(kulia) ambaye ni mwombaji wa mkopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 katika
ofisi za HESLB jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Septemba 2, 2015).
HESLB inaendelea na kazi ya kurekebisha taarifa za wanafunzi waliokosea
kujaza fomu zao za maombi. (Picha na Eline Maronga-HESLB)

Afisa
wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bi. Zahra Kitara
(kushoto) akipokea viambatanisho vya maombi ya mkopo kutoka kwa Bw.
Paul Yahhi (kulia) mwombaji wa mkopo ambaye fomu yake ya maombi
ilikosekana baadhi ya viambatanisho jijini Dar es Salaam leo (Jumatano,
Septemba 2, 2015). HESLB inaendelea na kazi ya kurekebisha taarifa za
wanafunzi waliokosea kujaza fomu zao za maombi. (Picha na Eline
Maronga-HESLB).

Maafisa
wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) (kulia)
wakiwahudumia waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 ambao
fomu za maombi zimegundulika kuwa na upungufu jijini Dar es Salaam leo
(Jumatano, Septemba 2, 2015). HESLB inaendelea na kazi ya kurekebisha
taarifa za wanafunzi waliokosea kujaza fomu zao za maombi.

Waziri wa
Fedha Saada Mkuya Salum akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi wa Serikali na wajumbe kutoka Benki ya Exim ya Korea baada ya
kusaini hati ya mkataba wa makubaliano ya mkopo wa Dola za Kimarekani
milioni 91.032 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 154.39 za Kitanzania
zilizotolewa na Benki ya Exim ya Korea kwa ajili ya ujenzi wa daraja la
Salenda jana jijini Dar es salaam.(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

Kaimu
Mkurugenzi wa TAMWA Edda Sanga akiongea kuhusu ilani ya Mtandao wa
wanawake wa katiba na uchaguzi iliyozinduliwa hapo jana katika viwanja
vya TGNP Mabibo, Dar es salaam. Wanaofuata ni Mwakilishi wa TAWLA,
Mkurugenzi wa TGNP Lilian Liundi na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha
Mafunzo ya Jinsia (GTI) Asseny Muro.
ILANI YA UCHAGUZI YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA NA UCHAGUZI
UCHAGUZI MKUU 2015
UTANGULIZI
Uchaguzi
wa mwaka 2015 ni wa kihistoria katika harakati za ukombozi wa mwanamke
nchini Tanzania. Mwaka huu tunatimiza miaka 20 tangu serikali wanachama
wa Umoja wa Mataifa zikubaliane kuwa na ”Mpango Kazi’’ wa Kumkomboa
Mwanamke ujulikanao kama Mpango Kazi wa Beijing (Beijing Platform of
Action) ambapo Mtanzania GetrudeI.Mongela alikuwa Katibu Mkuu. Mpango
huu uliainisha masuala 12 ya kipaumbele ikiwa ni pamoja na ushiriki wa
wanawake katika ngazi zote za uongozi, uwezeshaji wa kiuchumi,
uwezeshaji kisheria, haki za afya ya uzazi, haki za mtoto wa kike na
uondoaji wa mila potofu. Miaka 20 ya Beijing, wanawake wa Tanzania tuko
wapi katika nyanja ya siasa na uongozi? Tunaelekea wapi ? Ndio maana
tunataka agenda ya uwezeshaji wa wanawake iwe kipaumbele
kitakachozingatiwa katika uchaguzi Mkuu 2015. Pia ni mwendelezo wa
harakati zetu za kudai mabadiliko ya Katiba Mpya ambapo madai 12 ya
wanawake yaliwasilishwa.

MC’s
during the official opening of MultiChoice Africa Content Showcase
Extravaganza, IK (right) and Eku at the Outrigger Beach Resort in
Mauritius.(Photos by MultiChoice and Zainul Mzige of Modewjiblog).
It
was a magical night filled with #OnlyTheBest of African entertainment
when MultiChoice Africa kicked off its second #OnlyTheBest Content
Showcase Extravaganza in spectacular style at the Outrigger Resort.
The star-studded guestlist read like the who’s who of Africa’s entertainment and media.
The
guests walked down the African media Walk of Fame onto a red-carpet
that opened up to a sensational night of dazzling entertainment. The
event, dubbed ‘Night of a Thousand Stars’ saw all the glitz and glamour
of Hollywood, Bollywood and Nollywood come to life on the island
paradise, as guests that include Genevieve Nnaji, Rita Dominic, Desmond
Elliot and Ramsey Nuoah were given the full movie-star treatment.
Flavour, Stonebwoy and The Mavins kept the guests on their feet with
their popular hits while the night’s MCs IK and Eku kept the glamorous
proceedings running smoothly.
Guest
also experienced host IK who also brought his popular show, ‘High Lites
with IK’, to the stage in Mauritius with a delightful interview with
Nigerian crooner Banky W alongside music by DJ Sousa.

Red carpet treatment for the guest #OnlyTheBest.
Kutoka kushoto ni viongozi wa CEMOT, Meneja mradi, Bernard Kindoli na Balozi wa Den mack, Etnar Jensen.
Kutoka
kushoto ni Mwenyekiti mwenza kutoka Tanzania Civil Society Consortium on
Election Observation (TACCEO), Martina Kabisama, Meneja mradi, Bernard
Kindoli na Balozi wa Den mack, Etnar Jensen.
Wanahabari wakifuatilia mkutano huo.
Balozi wa Den mack, Etnar Jensen akitoa ufafanuzi baada ya kuulizwa maswali na wanahabari. (P.T)

Meneja
Uhusiano wa Airtel , Bwana Jackson Mmbando (Kulia) akimuonyesha Afisa
Mauzo wa Airtel Michael Nasare simu aina ya Samsung J100 iliyo na Selfie
Stick ya kupigia picha, wakati wa uzinduzi wa offa ijulikanayo kama
“Smartfonika Ujiselfonishe” inayowawezesha wateja kupata simu mbalimbali
za kisasa pamoja na kifurushi cha internet,sms na muda wa maongezi
bure.
Airtel
Tanzania, mtandao wa smartphone kwa kushirikiana na kampuni ya Samsung
leo imezindua offa kabambe ijulikanayo kama “smartphonika na ujiselfishe
na Samsung J100” itakayowapatia wateja wake simu mbalimbali za kisasa
za smartphone.
Akiongea
kuhusu ofa hii , Meneja Uhusiano wa Airtel , Bwana Jackson Mmbado
alisema “Hii ni moja kati ya ofa nyingi ambazo Airtel imetoa kwa wateja
wake kwa lengo la kuwawezesha kwenda sambamba na techonologia mpya na
simu za kisasa.(P.T)

Maandamano nchini Burundi
Watu wawili wameuawa katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura kufuatia makabiliano makali ya risasi Jumanne Usiku.
Kumekuwa
na machufuko zaidi katika wilaya zilizoadhirika kwenye maandamano ya
kupinga uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza wa kuwania muhula wa tatu.
Baadhi ya mitaa mjini humo zimezingirwa na maafisa wa ulinzi.
Nchini
Tanzania, idadi ya wakimbizi kutoka Burundi, inaendelea kuongezeka kila
uchao. Umoja wa Mataifa umesema kuwa wakimbizi mia nne kutoka Burundi
huvuka mpaka na kuingia Tanzania kila siku.
Kufikia
sasa zaidi ya wakimbizi elfu tisini wamekimbilia nchi jirani ya Tanzania
tangu mzozo wa kisiasa kuanza nchini Burundi, Aprili mwaka huu.
Idadi ya watu mashuhuri wanaouawa nchini humo imekithiri katika siku za hivi karibu.BBC
No comments:
Post a Comment