Kumefanyika mapinduzi nchini Burkina Fasso.
Kikosi
cha walinzi wa rais kimetangaza katika runinga ya taifa kwamba
kimevunjilia mbali kile ilichokitaja kuwa serikali ya mpito
isiyoambilika.Mwanachama wa kikosi hicho jenerali Gilbert Diendere ametajwa kuwa kiongozi mpya wa mpito.

Kikosi cha walinzi wa rais kimefyatua risasi hewani katika mji mkuu wa Ouagadougou huku watu wakikongamana kufanya maandamano.
Rais wa mpito Michel Kafando amepokonywa madaraka yake huku serikali yake ikivunjiliwa mbali, kwa mujibu wa afisa mmoja wa jeshi aliyezungumza katika runinga ya taifa nchini humo RTB.

Hatua hiyo inajiri baada ya viongozi wa serikali hiyo ya mpito nchini Burkina Faso kuzuiliwa na walinzi wanaomtii aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo Blaise Campaore aliyeng'atuliwa mamlakani.
Hakuna majeraha yalioripotiwa lakini kumedaiwa kuwepo kwa hali ya wasiwasi huku maduka yakifunga biashara mapema na raia wengi kuelekea majumbani mwao.

Bwana kafando na luteni kanali Zida walipewa jukumu la kuandaa uchaguzi mpya wa urais mwezi ujao.
Wao pamoja na maafisa wengine walitekwa nyara na walinzi wa RSP, mkuu wa bunge la mpito Moumina Cherrif Sy,alisema katika taarifa.
chanzo BBC
No comments:
Post a Comment